Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 12 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 12

 
Riwaya: SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA...
Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 12

Ilipoishia...

" Ooooh my daghter uko wapi mamaa siku zote hizo?. Alisema mzee edwad huku brayan nae machozi yakianza kumtoka..
" Ina maana bado uko hai?. Alisema mzee edwad.
" Mwanangu uko wapi mwanangu. Alisema jenipha akiwa analia.. Mwanangu umenifanyia nini mwanangu rudi mama mama yako nakufa mimi, umeniua mwanangu kwa nini umefanya hivyo jamaniiii Hiiiiiiiiiiiiii hiii hii hiiiiiii, Mwanangu najua ulikufa tukakuzika kabisa kumbe uko hai kwa nini walimwengu wako hivi mama jamaniii, kaburi lako kabisa lipo lucky lipo lipo lipo kumbe uko hai uko wapi kama hujafa mwananguu!!,, yuuuuuu mwanangu mimi, binti niambie ukweli mwanangu yuko wapi nimfatee mimi, nakufa mwana wa marehemu mimi jenipha jamaniii huuuuuuuuu, Ukoo wako wote unajua ulishakufa na kila siku tunaenda kaburini kwako siamini mimi siaminiii hiiiiiiiii hihihihiiiiiii..... alilalamika jenipha kwa kilio cha kupanda na kushuka huku mwanae brayan akimbembeleza aweze kunyamaza.


Songa nayo....

Maryam alikuwa katika kipindi kigumu cha mshangao sana kilichoambatana na maswali yasiyokwisha katika kichwa chake, hakufahamu wapi ashike wapi aache kwa jinsi alivyoona mapokezi ya familia juu ya lucky, alijiuliza inakuwaje wanajua amekufa wakati yuko mzima na kipi hasa kilifanyika hadi kujulikana amefariki.
Akili yake ilichanganyikiwa akashindwa la kufanya, aliona cha muhimu bora aage aondoke zake kuliko kwendelea, jenipha alimzua na kumuitaji waende wote chuo akamuone mwanae, mwaka na masiku kadhaa hajamtia machoni kitu ambacho ni kigumu kwa mzazi yoyote juu ya mtoto wake anaempenda.

" Mama brayan tulia kwanza mke wangu, maamuzi ya haraka sii busara inabidi tumsikilize binti kiundani kwanza ndo tuchukuane ikiwezekana familia kwenda huko. Alisema mzee edwad baada ya kumuona mkewe ana munkari wa hali ya juu wa kwenda kumuona mwanae.
" Naomba unyamaze baba brayan hujui kiasi gani naumia juu ya mwanangu, kila siku naenda kaburini kuweka maua kwa ajili yake kumbe namsulubu tu yuko hai?. Binti naomba twende chuoni nikamuone mwanangu siitaji kusikia chochote, awe mzimu, awe ndo yeye mzima, au copy yake, nataka nikamuone mwanangu, Twende binti. Alisema jenipha.
" Mama chuoni kwa kipindi hiki hairuhusiwi kwenda kuwaona wanafunzi bora nije nae nyumbani. Alisema maryam kwa sauti ya chini, macho yake tayari yalikuwa yanabubujikwa na machozi kwa kile alichokuwa anaendelea kukisikia, kichwa kilizingirwa na swali la kwa nini familia inajua lucky amefariki wakati yuko mzima?.
" Mwanangu naomba twende maprofesa wote wa chuo kikuu mimi wananifahamu hakuna anaeweza kunizuia kuingia. Alisema jenipha.nimesoma pale na mimi miongoni mwa wanafunzi wachache wa miaka ya 80 ambao hawawezi kusahaulika, nguvu zangu ziko pale na nina heshima kubwa kwa hilo usijali.

Maryam alitafakari ndani ya sekunde kadhaa, alijua kwenda na mama huyo bila kumtaarifu lucky yanaweza kuwa matatizo kwa upande wa wake mbali na mambo ya kichuo, alishamuelewa vizuri lucky kwa kipindi kifupi alichounga nae urafiki, aliamini anaweza kuchezea mkong'oto wa nguvu mtu mwenyewe akili ni ziro kichwani, lakini aliona potelea kote hawezi kuona kilio cha mama huyo kinaendelea kutoka juu ya kumuona mwanae kisha akaendelea kumgomea, alimkubalia wakasimama na kuanza kupiga hatua za kutoka jenipha akiwa na nguo za nyumbani bila kubadilisha.
" Mama brayan mbona hutumii akili wee mwanamke rudi kwanza tupange namna ya kwenda. Alisema mzee edwad akionekana kusikokubaliana na uamuzi wa mke wake. Maneno yake yalimfanya jenipha asimame kisha ageuke nyuma, alimwangalia mmewe kwa jicho chungu akamwambia.
" Ikiwa huna uchungu na damu yako ni wewe mwenyewe, miezi kumi na nne sasa nateseka juu ya kifo cha mwanangu, sikuruhusiwa hata kumuona alipofariki na kifo chake kilikuwa cha kutatanisha, nimekuwa wa kushinda makaburini kama mjane nlofiliwa na mume, nliomba kila nlipopata nafasi ya kuomba ikiwezekana afufuke aje aniage, niacheni kama nlivyo mkitaka mtakuja msipotaka bakini lakini mimi naenda. Binti twende. Alisema jenipha wakafungua mlango na kutoka ndani, mzee edwad na mwanae brayan waliangaliana wakakunja nyuso zao.
" Kwa nini hakufa?. Aliuliza mzee edwad.
" Hii ishu atakuwa aliifanya mzee mjunile mwenyewe, kumbuka alisema nguvu ni ndogo inabidi tutoe mali afanye uchunguzi mwengine kwa njia nyengine sijui kama ilikuwa ndani ya mkataba.
" Wapigie vijana waende kummaliza huyu binti kabla ya kufika huko chuoni ikiwezekana wamteke na huyu bibie ( jenipha ) kabisa, itakuwa aibu kubwa sana itayopelekea vifo vyetu ikiwa mikakati yote iliyo siri itajulikana. Alisema mzee edwad.
" Inasikitisha sana baba, siamini kama huyu dogo yuko hai kabisa, kwa sababu mbali na mambo ya mzee mjunile nlimtandika risasi mimi mwenyewe tena ya moyo. Alisema brayan.
" mpigie kijana wa getini aangalie namba za gari kabla haijatoka, wapigie wakina Suma waifatilie na kuikwamisha kabla haijafika chuo, na nadhani itakuwa bora zaidi kama tutaenda kumuulia mbali mzee mjunile.
" Ni kweli kabisa baba. Alisema brayan akipiga namba ya kijana wa getini Kaiza. Baada ya kuita na kupokea alimwambia aziangalie kwa makini namba za gari inayotoka muda huo kisha amwambie, kaiza alifanya alichoambiwa akaangalia gari na kuwapatia namba zake T 253 AH, brayan alikata cm akawapigia vijana wengine waliokuwa vijana wa kazi ili waende kuikwamisha hiyo gari isiweze kufika katika makazi ya chuo kikuu cha dar es salam...

Sebleni walikuwepo wawili tu madada wa kazi na wao walishaenda kwendelea na kazi zao, walichoitaji ikiwa lucky yuko mzima basi kisijulikane chochote kile kilichoko nyuma ya pazia, hata kama ni vita wainzishe wafe wao au wengine lakini kuhakikisha siri iliyopo kati yao na lucky inaendelea kuwa siri na mama mtu hajui chochote kwani kujua kwake kutakuwa ni hatari kwao ambapo wanaweza kufunguliwa mashtaka ya hukumu ya kifo kwa mujibu ya kifungo cha sheria namba 901 cha mwaka 1980.
Maryam na jenipha waliingia kwenye gari mbio mbio na kuianza safari ya kuelekea chuoni, kaiza getini alishangaa sana namna gari lilivyotoka huku bosi wake akionekana kuwa rafu rafu.
" Mmh nna wasi wasi huko ndani kishanuka, na kama kimenuka kibarua changu kimeota nyasi. Ila huyu mama aliharibika kisaikologia tokea kifo cha precious kitokee, inaonekana kuna mambo tayari yako nje nje huko. Alisema baada ya kufungua geti na kufunga.

Gari ya maryam iliyokuwa aina ya prado new model yenye usajili wa namba T 253 AH ilipiga masafa ya mbio kuelekea chuo, huku mzee edwad na mwanae walionekana kuchanganyikiwa sana kwa kilichotokea.
" Inakuwaje huyu mtoto hakufa jamani mbona tutauana kwa presha?. Alisema mzee edwad, tumbo lilikuwa joto, sura ilishakunjamana ikakaa kishari, hakuwa mzee sana alikuwa kwenye miaka 50 kamili, meno aliyatafuna mdomoni kwa hasira akapagawa.
" Mimi naamini mambo yote yataenda sawa tu baba, umepita mwaka sasa hakuna alieweza kuijua hii ishu, cha kufanya hapa inabidi tutumie roho ya paka, huyo binti auawe alieleta hizo taarifa na kuamsha vidonda vilivyopona, mama mambo mawili yamkute, kifo, au tumfanyie kitu kibaya kitachomfanya apoteze kumbu kumbu zote za nyuma. 


Alisema brayan kumshauri baba yake, mbinu aliyoipanga juu ya mama yake ni kama hakuwa mama yake wa kumzaa, aliona bora afe au apoteze kumbu kumbu kuliko mambo yao kuharibika.
" Umeongea point moja nzuri sana, ndo maana huwa nakuaminia jembe langu sikupoteza mbegu nlipokuzaa kijana una akili sana. Alisema mzee edwad akaendelea kusema. Shika funguo Kachukue vifaa vya moto chumbani kwangu, unichukulie na ile kofia yangu tutoke twende kwa huyu mzee mjunile kwanza akatueleze vizuri. Alisema mzee edwad brayan akainuka kwenye kiti na kwenda hadi chumbani kwa baba yake, alipatiwa funguo ya droo ambayo huwa haigusi mtu yoyote zaid yake, alipofika alifungua akatoa silaha mbili aina ya miguu ya kuku bastola, kisha alifunga akachukua na kofia aliyoambiwa na kurudi sebleni.
Kati ya wafanyakazi wawili wa ndani wote hawakuwa wakijua kinachoendelea, walichokuwa nacho ni cha lucky kuwa hai kitu ambacho na wao kiliendelea kuwaumiza akili, mzee edwad alisimama sebleni akaweka suti yake sawa akavaa na kofia yake ambayo huwa anaitumia katika mambo yake ya siri ili kumficha sura, ilikuwa ndefu kidogo anapoivaa hata ukikutana nae huwezi kumjua mpaka aitoe, yeye na mwanae walitoka wakashuka hadi chini ambako waliingia kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea kwa mzee ambae ilionekana waliongea nae dil na kwa lilivyoenda wakahisi yeye ndo amefanya usaliti...


Ndani ya mchuma wa prado aliyokuwemo maryam na jenipha hakukuwa na mazungumzo yoyote zaid ya huzuni, Maryam alikuwa kwenye hatari kubwa sana ya kupoteza maisha kwa kuyaingilia maisha ya watu kisa kumsaidia mtu, jenipha machozi yalikuwa yanamtoka maryam hakupata chansi ya kumuuliza chochote, aliendesha gari kwa makini akafanikiwa kufika sheri ambako kuna bara bara ya kwenda katika chuo cha ardhi, mafuta tayari yalipungua ndani ya gari ikabidi apinde aingie sheri, aliweka mafuta ya elfu 50 akakanyaga gia na kwendelea mbele, walitumia dakika tano wakitokea bara bara inayotokea mwenge wakafika kulikokuwa na mataa ya kusimamisha gari na wao ikawabidi wasimame zilikuwepo nyekundu, walikuwa wapindie kushoto waifate bara bara inayoelekea chuo hivyo ilibidi wasubiri taa ya kijani itayoonesha mshale wa kuelekea kushoto kukatiza bara bara ya pili ya kutoka ubungo kwenda mwenge iwake.
" Mama pole sana kwa matatizo yaliyoko mbele yako. Alisema maryam baada ya kusimamisha gari na kumwangalia jenipha huku akipiga jicho juu ya mataa kama yashawaka au laa.
" Asante mwanangu, nimekuwa wa kuteseka kwa kipindi cha mwaka sasa mimi!, nali kila leo, mwanangu maiti yake sikuruhusiwa kuiona zaidi ya mara ya mwisho akiwa hospitalini, na jeraha la risasi ambalo sikujua amelipata kwa nini?. Alisema jenipha akiwa ameegamia kiti, rundiko la machozi likiwa usoni mwake.
" Ina maana lucky aliwahi kupigwa risasi?. Aliuliza swali la mshangao maryam.
" Ndio!, sikujua kwa nini ila uenda ni kwa sababu watu wengi walikuwa hawampendi mwananguuu!, na nlimwambia mimi lucky badilika maamaaa utaniweka kwenye matatizo mama yako lakini hakutaka kusikia, Huuuuuuuuuuu mwanangu mimi jamaniiiii!!.

Alisema jenipha na kipindi hicho hicho taa zikawa zinaruhusu, kitendo cha gari yao kuvuka upande wa pili tu kuna gari nyeusi kubwa iliyokuwa inatokea upande wa bara bara ya ubungo, iliwasababishia ajali ya maksud ambayo ni kama tayari ilidhamiriwa, iligonga kioo cha mbele upande aliko jenipha jenipha akapata mshtuko na kuzimia hapo hapo, maryam alifanya utaratibu wa kuirudisha nyuma gari baada ya kugongwa bila kujali nyuma yake kuna nini, lakini kabla ya kufanya hivyo zilimiminwa risasi za kufa mtu katika gari hilo zikitokea kwenye gari lililosababisha ajali, raia walioliona hilo walianza kutawanyika ovyo ovyo kuingia mafichoni, risasi zilimiminika ndani ya dakika moja kisha gari likawasha mafuta na kuondoka zake, haikuwa vyepesi kujulikana kama kuna aliepona kati ya jenipha na maryam, hata baada ya watu waliosababisha kuondoka raia waliogopa kusogea kitu kilichokuwa hatari zaid kwani hata kama alikuwepo aliepona kati ya wawili hao angekufa muda wowote kwa kucheleweshwa kuwahishwa hospitalini.

NINI KITAENDELEA KATIKA EPISODE YA 13 ? Kesho pita kwenye App yetu kupata uhondo zaidi. Kama bado hauna App yetu >BOFYA HAPA< Kuipakua kwenye Simu yako.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.