Shamsa Atoa Siri ya Wasichana Kushindwa Kudumu Kwenye Mahusiano - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shamsa Atoa Siri ya Wasichana Kushindwa Kudumu Kwenye Mahusiano

Msanii wa bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kuweka wazi sababu za wadada wengi wa mjini kushindwa kutokuolewa wala kutokudumu katika mahusiano yao.shamsa anasema kuwa wadada wengi hasa wasanii wamekuwa na tabia ya kuingiza umaarufu wao katika mahusiano kitu kinachofanya washindwe kudumu katika mahusiano yao.

"Nimegundua mahusiano mengi ya watu aarufu hayadumu kwa sababu wengi wanataka ustar hadi kwenye mahusiano , hata mtu wa kawaida akiwa katika mahusiano na msanii pia inakuwa kazi kwa mahusiano yao kudumu kwa sababu hiyo.

Hasa kwa wanawake tunaamini kabisa ustar ndio kila kitu katika mahusiano na mwanaume , sijui ni kwa sababu hatuna elimu ya ustar au vipi, maana ingekuwa u-star shida Beyonce na Jay -Z wasingekuwa wamedumu katika ndoa maana hawa ndo ma-star wa Dunia."


Shamsa ni moja ya wasanii wachache wa kike walioweza kudumu katika ndo yao na mume wake tangu mwaka 2016 alipofunga ndoa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.