Sare za Sekondari Zamtoa Macho Snura - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sare za Sekondari Zamtoa Macho Snura

Staa wa miondoko ya mduara bongo, Snura Mushi amefunguka kuwa amejikuta akizitolea macho sare za wanafunzi wa sekondari baada ya kuishia kuvaa za shule ya msingi kutokana na uwezo duni waliokuwa nao wazazi wake.

Snura au Mamaa Majanga aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, huwa anawaasa wasichana kwamba wamepata fursa ya kusoma, watumie nafasi hiyo kwa sababu yeye hakubahatika kabisa kukanyaga sekondari wala kuvaa sare hizo, jambo ambalo linamfanya sasa hivi atumie nguvu ili wanaye wapate elimu.

“Kiukweli nikiona wasichana wamevaa sare za sekondari huwa ninazitolea macho sana. Natamani siku zirudi nyuma ili nami nipate elimu hiyo,”
alisema Snura aliyeishia darasa la saba.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.