Sarah Umwambii Kitu kwa Harmonize Aonyesha Jeuri ya Pesa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sarah Umwambii Kitu kwa Harmonize Aonyesha Jeuri ya Pesa

Penzi la Harmonize na mpenzi wake, Sarah bado ni moto, tena wa kuotea mbali.

Safari hii Sarah amemuonyesha Harmonize ni kwa namna gani anampenda kwa kumnunulia saa ya mkononi ambayo inatajwa kuwa ya gharama zaidi.

Katika ukurasa wake wa Instagram Harmonize aliweka kipande kifupi cha video kinachoonyesha saa hiyo na kumshukuru Sarah kwa zawadi kama hiyo na kuwataka wanaohitaji kujua gharama yake kuitafuta mtandaoni.

Saa aliyozawadiwa Harmonize inajukalikana kwa jina la Patek Philippe, saa hii katika mtandao inaoneka kuuzwa kati dola za Kimarekani 78,999 hadi 119,999. Sawa na kati ya Tsh. 177,948,749 hadi 270,308,693.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.