RayVanny Atangaza Ndoa Afuata Nyayo za Diamond - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

RayVanny Atangaza Ndoa Afuata Nyayo za Diamond

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka WCB Rayvanny amefuata nyayo za Bosi wake Diamond Platnumz aliyetangaza kufunga ndoa mwaka huu ambapo na yeye amesema tegemea kuona ndoa yake hivi karibuni.

Diamond aliwashangaza watu siku chache zilizopita baada ya kumuomba Baraka mama yake mzazi na kumuhaidi kuwa atafunga ndoa mwaka huu hasa kwa sababu ameachana na mpenzi wake Zari mwezi uliopita.

Lakini inaelekea Rayvanny amefuata nyayo hizo hizo kwani na yeye ameibuka na kusema kuwa na yeye anatarajia kumuoa mpenzi wake na mama watoto wake Fahyma.

Taarifa hiyo imekuja siku chache baada ya wapendanao hao kutoka mkoani Mbeya nyumbani Kwa Rayvanny ambapo walienda kwa ajili ya shughuli zao za kifamilia.

Kupitia mtandao wa Instagram Rayvanny aliweka picha yake akiwa katika vazi la suti na kuandika “Bwana Harusi” naye mpenzi wake Fayvanny hakubaki nyuma na akuamua kujibu kuashiria wapo katika michakatao hiyo ya ndoa.

"Ohh bby I can’t wait for the day & you will be mine forever (sooooooon) @rayvanny "

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.