Rayvanny Afunguka Mazito Kuhusu Diamond Platinumz - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rayvanny Afunguka Mazito Kuhusu Diamond Platinumz

Msanii Rayvanny amefunguka na kuzungumzia yale anayoyapitia bosi wake  ( DIAMON PLATINUMZ )  na kumwambia kuwa hakuna mafanikio ambayo hayana changamoto wala kukosa maadui.katika ukurasa wake wa instagram Rayvanny aliandika:-
 Kuna vitu pengine unaweza kuwa unapatia au unakosea , sitaki kuongelea hiloswala kwa sababu wewe pia ni binadamu.ILA KWNYE KUSEMA UKWELI NITASEMA sio kwa sababu wewe ni boss wangu hapana !!ila mara nyingi thamani ya mtu  na umuhimu wa mtu watu huwa wanajua pale ambapo anakuwa amondoka.MUZIKI NI KAZI NA NI AJIRA  namaanisha kuwa kuna familia nyingi tu zinaishi kupitia huu mziki.
 DIAMOND KATIKA WASANII WOTE  wewe umekuwa ni msanii wa kuongeza chachu kwa wasanii wengine, na kupitia wewe naamini kuwa wengi wamefanikiwa , KUJITOA KWAKO NA KUAMINI KATIKA UMOJA  NA PIA KUTHUBUTU ndipo kulikokufanya  unafanikiwa….USHAAMBIWA KUWA HAUJUI KUIMBA lakini uliimba na ukafanikiwa, ULISHAAMBIWA UNAVIMBA UNAIGIZA  MAISHA lakini sasa unayaishi hayo maisha ..hakuna aliyefanikiwa akakosa maadui ndivyo dunia ilivyo…

MIMI ULINISAIDIA ULIJUA SHIDA ZANGU naaminikuwa mungu alikutumia  wewe ukawe mkombozi wangu  KWAIO KUMBUKA KUWA ILI MBEGU ITE LAZIMA IOZE…. SINA MUDA  WA KUMSMA MTU ILA FANYA KAZI SIMBA

Hivi karibuni diamond aliingia katika vita na Naibu waziri kwa sababu ya kufungiwa kwa nyimbo zake mbili , na pia hivi karibuni alifunguka na kusema kuna watu na media zipo kwa ajili ya kuua muziki wake na lebel yake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.