Queen Darleen Amkana Alikiba Kweupe Kabisa. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Queen Darleen Amkana Alikiba Kweupe Kabisa.

Mwanadada Queen Darlen ameamua kufunguka na kusema kuwa hana ukaribu wowote na Alikiba zaidi ya kwamba walikuwa wakifanya kazi pamoja na hiyo yote ilikuwa ni kwa sababu walikuwa chini ya uongozi unaofanana.Queen Darleen amesema huwa anapoulizwa na media kuhusu Alikiba hapendi kumzungumzia kwa madai kuna watu watatafsiri tofauti.

Wasanii hao ambao mwanzoni watu walidhani ni ndugu walishafanya wimbo pamoja na Queen Darleen amesema ni kwasababu kipindi hicho yeye na Alikiba wote walikuwa chini ya label moja. Queen Darleen amesema Hana ukaribu wowote na Alikiba tangu zamani ilikuwa ni kazi tu.

Pia akizungumza Global Queen Darleen amesema wakati anaanza muziki takribani miaka 15 iliyopita hakupata usumbufu wa rushwa ya ngono toka kwa wanaume walio kwenye tasnia Kama baadhi ya wasanii wa kike kwasababu yeye alishikwa mkono na Dully Skyse kwa hiyo akizinguliwa tu kwa mambo ya kijinga alikuwa akimwambia Dully.

- GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.