Penny: Ningemzalia Mtoto Daimond Lakini... - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Penny: Ningemzalia Mtoto Daimond Lakini...

Penny: Ningemzalia Mtoto Daimond Lakini....
KITAJA orodha ya mastaa wa kike Bongo ambao siku za nyuma walisumbua kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, basi huwezi kuacha kutaja jina la Mtangazaji wa Kipindi cha Harusi Yetu kinachorushwa kupitia Televisheni ya Magic Swahili, Penniel Mungwilwa ‘Penny’.

Mtangazaji huyo alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa Afro-Pop mwenye jina kubwa ndani na nje ya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kabla ya kumwagana. Penny aliingia kwenye uhusiano na Diamond huku akijua kuwa jamaa huyo alikuwa ni shemeji yake kwa staa mkali wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ambaye walikuwa ni mashosti.

Penny amefanya mahojiano maalum ya ana kwa ana na Ijumaa Wikienda na kufungukia tetesi zinazosambaa kuwa amerudisha majeshi kwa Diamond na ndiye mkewe mtarajiwa;

Over ze Weekend: Ukimya wako Penny unawapa hofu mashabiki wako, kulikoni?

Penny: Siyo kwamba niko kimya, bali unapokuwa busy na kazi, watu wanajua labda haupo maana mambo ya huku na kule unakuwa huna.

Over ze Weekend: Hivi karibuni ulitupia picha mbalimbali kwenye ukarasa wako wa Instagram ambapo mashabiki wengi walikupongeza na kusisitiza kuwa wewe ndiye mrithi wa Madale (nyumbani kwa Diamond) baada ya Zari kubwaga manyanga, unalizungumziaje hilo?

Penny: (Kicheko) unajua hao ni mashabiki, wana uwezo wa kusema chochote wanachokifikiria akilini mwao na huwezi kuwakataza kwa sababu wana uhuru wa kuniambia chochote.

Over Ze Weekend: Lakini pia dada wa Diamond, Queen Darleen naye alitupia picha yako kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo ilizua gumzo kuwa umerudisha mapenzi kwa kaka yake, je, nini mtazamo wako?

Penny: Kwanza ikumbukwe kabisa Darleen ni rafiki yangu sana tangu kitambo. Kufanya hivyo sioni kama ni tatizo kabisa kwa sababu familia yote ya Diamond sina tatizo nayo, lakini kurudiana na Diamond siwezi.

Over Ze Weekend: Kwa nini huwezi?

Penny: Kwa sababu alishakuwa na maisha yake mengine ya kimapenzi na mimi hivyohivyo.

Over Ze Weekend: Kwa hivi sasa inajulikana wazi kuwa Diamond ameshaana na Zari, je, akijipanga kuja kutoa posa kwenu utaridhia?

Penny: Siwezi kukubali kuolewa naye hata siku moja maana mapaenzi yalishaisha, hayapo tena.

Over Ze Weekend: Kwa kuwa Diamond ametangaza kuoa mwaka huu, nini ushauri wako juu ya amuoe nani kati ya Hamisa, Zari na Wema ?

Penny: Kwa mimi wa kumuoa hapo kwanza yeye angalie mwanamke anayempenda kwa dhati, anayejua kuangalia familia na kumshauri vyema katika kazi zake na pia asithamini sana starehe badala ya maendeleo.

Over Ze Weekend: Mastaa wengi sasa hivi wamejaliwa watoto na pia wanajivunia, vipi kwa upande wako?

Penny: Hata mimi napenda mtoto pia, lakini kamwe nilishaapa lazima nizae na mwanaume wa malengo na baba bora.

Over Ze Weekend: Kwa hiyo kipindi uliposhika mimba ya Diamond na ikachoropoka alikuwa ni baba bora?

Penny: Siwezi kusema sana, ningemzalia, lakini bado alikuwa na mambo mengi.

Over Ze Weekend: Kipindi cha nyuma ulikuwa na bifu na Wema baada ya kuwa na Diamond, lakini mlilimaliza ila hamjawahi kuonekana pamoja hata siku moja kwenye ishu yoyote, kulikoni?

Penny: Hapana…hatuna tatizo lolote, ila imetokea yeye anakuwa na kampani yake na mimi hivyohivyo na tunapokutana tunafurahiana sana.

Over Ze Weekend: Kuna madai kuwa mara nyingi unapokuwa na mpenzi akikuudhi huchelewi kunywa sumu, je, hili likoje?

Penny: (Anaguna)…hao watu sasa wanaongeza chumvi, kwa hiyo hata mtu akilazwa hospitalini akisumbuliwa na ugonjwa fulani watasema sumu?

Over Ze Weekend: Asante Penny kwa usahirikiano wako.

Penny: Karibu, nawapenda wasomaji wa Ijumaa Wikienda na ndilo gazeti langu, siwezi kulikosa kila Jumatatu. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.