Nandy Aweka Wazi 'Sina Mpango Wa Kufanya Kolabo na Ruby' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nandy Aweka Wazi 'Sina Mpango Wa Kufanya Kolabo na Ruby'

Maanamuziki wa Bongo fleva kutoka katika nyumba ya vipaji Tanzania (THT) Nandy amefunguka kuhusu uhusiano wake na msanii mwenzake Ruby na kusema bado hakujawa na mipango ya kufanya kolabo

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi za kuwepo kwa bifu kati ya Nandy na Ruby huku tetesi hizi zikichochewa zaidi na aina ya muziki wanaofanya huku kila mmoja akikataa kufananishwa na mwenzake.

Hivi karibuni Nandy alikaaa chini na Sam Misago Tv na aliulizwa kama ana mpango wowote wa kufanya kazi na Ruby baada ya kurudi THT.

Nandy amefunguka na kuweka wazi kuwa kwa sasa hakuna mipango yoyote au mikakati iliyopangwa kwa ajili ya kupiga kolabo.

Haijawa kwenye plan wala sijawahi kufikiria kufanya hivyo lakini inawezekana ikatokea kama mashabiki wakihitaji na management ikiamua”.

Lakini pia Nandy amesisitiza kuwa hana bifu na Ruby na wala hajawahi kuwa na bifu naye na akisikia watu wanasema hivyo hashtuki Tena kwani ameshazoea kwa sasa.

PIGA MAPESA KIULAINI SASA INGIA >>HAPA<< SASA

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.