Mwana FA Aungana na Mourinho - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mwana FA Aungana na Mourinho

Msanii wa HipHop Bongo, Mwana FA ambaye ni shabiki maarufu wa klabu ya Manchester United ya England ameunga mkono kauli ya kocha wa timu hiyo Jose Mourinho, kuwa nyota Alexis Sanchez hatakiwi kulaumiwa kwa kiwango chake ndani ya muda mfupi.

Hivi karibuni Mourinho alisema kuwa wanaomlaumu Sanchez kwa kutoonesha kiwango kikubwa tangu asajiliwe msimu huu hawatakiwi kufanya hivyo kwani bado ana muda zaidi na yeye kama kocha analijua hilo na atalifanyia kazi.

Kwa upande wa Mwana FA yeye amesema Sanchez hatakiwi kulaumiwa kwani uzuri wa mchezaji muda mwingine huonekana timu ikiwa inafanya vizuri hivyo uwezo wa Sanchez utajieleza tu timu ikianza kufanya vizuri, kwasababu anajulikana ni mchezaji wa kuamua matokeo.

Aidha Mwana FA ameongeza kuwa yeye anaamini katika kuwapa wachezaji muda na suala la Sanchez limekuwa kama ilivyokuwa kwa nyota mwingine Paul Pogba ambaye alionekana kutofanya vizuri katika msimu wake wa kwanza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.