Mimi Mars: Sitaki Kuolewa na Mwanaume Mpare - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mimi Mars: Sitaki Kuolewa na Mwanaume Mpare

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Papara’ Mimi Mars ambaye pia ni mdogo wa staa wa Bongo fleva Vanessa Mdee, amefunguka na kuweka wazi kuwa hataki Kuolewa na mwanaume kabila la Wapare.

Mimi Mars amesema kuwa hategemei na wala hataki kuolewa na mwanaume kutoka katika kabila la wapare kwa sababu yeye mwenyewe ni mpare na kuna baadhi ya tabia za wapare anazijua na hazimpendezi.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Mimi Mars pia ametaja Makabila mengine kama wachaga ambayo nayo amekiri hatorudia Tena kuwa nao:

"Kwa sababu mimi mwenyewe ni mpare kwaiyo tabia za wanaume wa kipare kidooogo nazijua alafu wanasemega ile mafahari wawili hawawezi kukaa kwenye zizi moja kwaiyo najua tutashindwana tu maana wote ni wabishi, wabahili kwaiyo tutashindwana tu na sio kwa ubaya ila mimi tu sipendi."

Lakini pia Mimi Mars ameweka wazi kuwa kwa sasa hana mpenzi yupo single:

"Hapana mimi sahivi sina mtu niko peke yangu sina mchumba"

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.