Mbasha Amtolea Uvivu Mwanamke Aliyedai Ana Mimba Yake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mbasha Amtolea Uvivu Mwanamke Aliyedai Ana Mimba Yake

MSANII wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha, amefunguka na kuwatolea uvivu mabinti wa Bongo akisema wengi wao hawaolewi kwa sababu wamekuwa wakiwaza zaidi kuhusu starehe na si maisha yao ya baadaye huku akidai ndiyo sababu ya vijana wengi kuoa wanawake wakubwa au ambao wamekomaa kiakili na wanaowaza maisha na si starehe.

“Vijana wa sasa wame-focus kwenye maisha zaidi, hivyo wanahitaji mwanamke aliyekomaa ubongo ambaye wanaweza kufanya mipango ya maisha na kupaa kwa pamoja hadi kwenye ndoto zao. Hii ndiyo inapelekea wanawake wenye umri mkubwa kuolewa kwa kasi kubwa. Hivi vichenchede vinavyowazia kubandika kucha na kope bandia na kusingizia mahusiano ya uongo ili kupata kiki na mimba hewa sasa havina soko vimebakia kuchuna viinua mgongo vya wanajeshi wastaafu,” alisisitiza Mbasha.

Hivi karibuni taarifa zilisambaa mitandaoni zikisema mwanamitindo, Agness Martin ‘Agness’ yupo kwenye mahusiano na Mbasha na kuwa ndiye mwanamume ambaye yuko mbioni kuzaa naye mtoto hadi kufikia hatua ya kufuta Followers wake wote Instagram na kumuacha Mbasha pekee.

Licha ya taarifa hizo kusambaa huku akiweka picha ya mwanamke aliyetoka kujifungua na kuandika maneno kuwa anatamani kuzaa, Agness alikanusha taarifa za kuwa na mahusiano na Mbasha na kusema wao ni wasanii tu na wanaheshimiana, hawawezi kufanya kitu kama hicho.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.