Mama Uwoya Amkana Dogo Janja, Adai Hatambui Ndoa Yao - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mama Uwoya Amkana Dogo Janja, Adai Hatambui Ndoa Yao

Mama mzazi wa msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hatambui kuhusu ndoa ya mtoto wake na msanii mwenzake Dogo Janja na kusema kama wamefunga ndoa wanaijua wao ila yeye na baba mzazi wa Irene hawaitambui.

Mama mzazi wa Irene Uwoya ameweka wazi hilo alipokuwa akifanya mahojiano na moja ya chombo cha habari na kusema kuwa yeye na baba wa Irene hawaitambui hiyo ndoa ya mtoto wao na Dogo Janja.

"Kwanza huyo kijana sijui niongee lugha gani mimi nilishaongea toka mwanzo na nilisema nadhani wote mlishuhudia hata kwenye msiba wa mkwe wangu Irene alikuwa bado kwenye ndoa sasa wao kama wamefunga ndoa yao wanaijua wao mimi na baba yake mpaka leo hatuijui hiyo ndoa, mimi kwanza hata sijawahi kumtia machoni huyo kijana sasa sijui kama anasema alikuja kujitambulisha simjui huyo mzazi wake na sielewi aliowaozesha ni kina nani, labda ana wazazi wengine na ndugu wengine na hao ndugu anaosema walidhuria kwenye harusi yake ni kina nani ?

Mzazi huyo wa Irene Uwoya aliendelea kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo;

"Anavyosema hajabadili dini mimi sijawahi kuona Muislam akafungisha ndoa ya mmoja Mkristu mwingine Muislam, nachofahamu mimi kwenye dini ya Kislamu huwezi kufunga ndoa ya mseto lazima ubadilishe dini kwa hiyo aeleze vizuri kama amebadili dini kwanini anaficha, ila kama amebadilisha dini yeye ni mtu mzima na sisi wazazi hatuwezi kuhusika hapo. Ila yeye na huyo mume wake hatujawahi kuwaona hapa nyumbani. Ila mimi malumbano na mtoto niliyemzaaa sipendi na sina tatizo lolote na yeye atabaki kuwa mtoto wangu lakini sipendi kuingizwa kwenye vitu vya kipuuzi" alisisitiza Mama Irene.

-udakuspecially 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.