Mama Kanumba Aangua Kilio Stendi ya Mabasi Dar - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mama Kanumba Aangua Kilio Stendi ya Mabasi Dar

MAMA wa aliyekuwa mwigizaji kinara wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, kama kawaida yake ameangua kilio cha nguvu kwenye Stendi ya Mabasi ya Segerea jijini Dar, baada ya kuona bango kubwa la mwanaye huyo kwenye duka moja eneo hilo.

Akizungumza na gazeti hili kwa uchungu, mama huyo alisema kuwa, siku hiyo alikuwa anakwenda kurekodi filamu maeneo ya Segerea na alipofika kituoni hapo, alishuka kwenye basi ndipo ndipo akakutana uso kwa uso na picha kubwa ya mwanaye huyo.

“Kila mara naziona picha za Kanumba kwenye mabango, lakini sijui ni kwa nini hii nilipoiona, imenifanya niishiwe nguvu,” alisema mama huyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.