Kwa Mara ya Kwanza Tangu Kufungiwa kwa Nyimbo Zake, Diamond Awashauri BASATA - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kwa Mara ya Kwanza Tangu Kufungiwa kwa Nyimbo Zake, Diamond Awashauri BASATA

Msanii wa muziki nchini Diamond Platinumz jana kwa mara ya kwanza amefunguka na kuongelea swala la kufungiwa kwa nyimbo zake na nyimbo za wasanii wengine wiki kadhaa zilizopita kwa madai ya kuwa nyimbo hizo hazina maadili na zimekuwa na maneno ya kupotosha wasikilizaji.

Diamond anasema kuwa nyimbo nyingi zimekuwa zikifungiwa kwa sababu ya tasfiri binafsi na sio kwa sababu zinakuwa na matatioz kama wanavyosema.Hata hivyo Diamond anasema kuwa nyimbo nyingi za wasani wa nje zimekuwa zikipigwa katika vyombo vya habari na kuzifungia za wasanii wa ndani ya nchi.

"Huwezi kuimba nyimbo ya mapezni na ukaacha kusema maneno ya kimahaba, huo ni uongo kwa sababu hautafikisha ujumbe unaokusudia. nyimbo kama waka waka na hallelujah nilizifanya nikifikiria kuwa nataka kuona na soko lingine watusikilize serikali lazima ielewei hilo. nakitu kinachoniuma zaidi ni kwamba zinafungiwa nyimbo zetu lakini za kina nick minaj zinapigwa, so ni lazima hilo nalo tuliangalie."


Diamond aliongea hayo kwa mara yake ya kwanza kufumguka tangu kufungiwa kwa nyimbo zake mbili ambazo zimetoka hivi karibuni na tena zote akiwa amefanya na wasanii wakubwa kutoka nje ya nchi,maneno hayo aliongea Diamond alipokuwa katika mahojiano na waandishi wa habari nchini kenya ambapo akikwenda kwa ajili ya kufanya uzinduzi wa album yake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.