Kisa Urafiki na Wema, Aunt Ezekiel Atoa Povu...Sikuwa Rafiki wa Zari - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kisa Urafiki na Wema, Aunt Ezekiel Atoa Povu...Sikuwa Rafiki wa Zari

Baada ya picha mpya kusambaa na kuonesha muigizaji Aunt Ezekiel akiwa karibu na Wema Sepetu, wafausi wa aliyekuwa mchumba wa Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wamemchachamalia Aunt kwa kumuita mnafiki hali iliyosababisha mrembo huyo aibuke na kutoa povu.

Akizungumza na Risasi Jumamosi hivi karibuni baada Zari kummwaga Diamond na yeye kuonekana ‘klozi’ na Wema, Aunt alisema wamuache na urafiki wake na Wema kwani yeye na Zari hawakuwa marafiki kama alivyo Wema.

“Sipendi kabisa watu wanavyoniongelea juu ya suala hilo la ukaribu wangu na Wema, waniache kabisa kwani sikuwa rafiki wa Zari na siwezi kumsema vibaya, Wema atabaki kuwa rafiki siku zote,” alisema Aunt.

Aunt alisema, kamwe hawezi kuhofia maneno ya watu kwani Wema atabaki kuwa rafiki yake bila kuangalia Diamond ana uhusiano na nani.

“Maneno ya watu hayawezi kuniweka mbali na Wema huu ni uamuzi wangu na siwezi kumtenga Wema kwa sababu nilikuwa karibu na Zari hayo ni mambo yao mimi hayanihusu,” alisema Aunt.

Hivi karibuni, Aunt na Wema walionekana kwenye pati ya Papii Kocha na Babu Seya iliyofanyika katika Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar ambapo walivaa magauni sare na kucheza pamoja.

Kabla ya Zari hajammwaga Diamond, Aunt hakuwa akionekana mara kwa mara na Wema tofauti na sasa jambo ambalo ‘wambeya’ wengi mitandaoni wamekitafsiri kitendo hicho kuwa ni cha kinafiki baada ya hivi karibuni Aunt kuonekana karibu na Wema.

- GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.