Johari Afunguka Safari Ya Kwenda Kumuona Lulu Jela - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Johari Afunguka Safari Ya Kwenda Kumuona Lulu Jela

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Johari Chagula amefunguka na kuongelea sababu zilizompelekea kutomtembelea Lulu gerezani mpaka leo ilhali alifungwa tangu mwaka jana.

Elizabeth Lulu Michael ‘Lulu’ alihukumiwa kwenda jela mwaka jana tarehe 13/11 kwa muda wa miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Muigizaji wa Bongo movie Marehemu Steven Kanumba.

Tangu Lulu ametupwa jela kumekuwa na taarifa nyingi juu ya nini kinaendelea kwa Lulu huko Lupango. Wasanii wengi waliokuwa na ukaribu na Lulu wamedai ni vigumu kwenda Kumuona jela kwani kuna sheria za kwenda hivyo wengi wao hawajamuona.

Johari amefunguka Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, na kusema tangu Lulu amefungwa hajawa za kwenda Kumuona wala kumuuliza hali kwani anaogopa kumuongezea machungu.

"Kiukweli tangu Lulu amefungwa jela sijawahi kwenda kumsalimia, kwa upande wangu naona unapokwenda kumtembelea ni sawa na kumuongezea machungu na ukweli zaidi hivyo mimi ndio naona na ndio maana nakuwa mzito kwenda”.

Lakini pia Johari amesema kiitendo kilichowapata wote wawili kumaanisha Kanumba kufariki na Lulu kufungwa kiliwaumiza watu wote.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.