Idris Sultan Adaiwa Kunasa Kifaa Kipya - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Idris Sultan Adaiwa Kunasa Kifaa Kipya

Mchekeshaji na mshindi wa Shindano la Big Brother 2014, Idris Sultan, anadaiwa kunasa kifaa kipya kutoka nje ya nchi anayetambulika kwa jina moja la Aya, ambaye ataziba nafasi ya mwanadada kutoka Bongo Movie, Wema Sepetu ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake.

Ijumaa limepenyezewa ubuyu na chanzo kwamba Idris, ameamua kumnasa Aya ambaye ana jina kubwa nchini Tunisia na kwamba ndiye mrithi wa Wema kwani tangu aachane naye hajapata mrembo mwenye jina kubwa kuliko yeye na aliyempenda kwa dhati.

“Nyie muulizeni tu Idris atawaambia. Sasa anakifaa kipya kutoka nje, kinaitwa Aya na hivi karibuni alitua Bongo wakafanya matanuzi hadi picha zingine zikasambaa wakiwa swimming pool wakiogelea kimahaba,” alisema sosi huyo.

Baada ya kutumegea ubuyu huo, Ijumaa liliweza kumsaka Idris,ambapo baada ya kupatikana alifunguka;
“Aya ni kweli ninamfahamu. Ni mtu wangu wa karibu saana lakini sina uhusiano naye wa kimapenzi. Tumekutanishwa na programu ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, na yeye alikuja Bongo kwa ajili ya kikao cha project hiyo,” alisema Idris.

Hata hivyo, gazeti hili lilizidi kumbana Idris, kwamba kukutana kwa ajili ya project ndiyo waonekana mpaka hotelini, kwenda kuogelea na kwenye mapozi tata kama mtu na mpenziye, ambapo alijibu kukutana huko kulitokana na ukaribu wao tu na si vingine.

“Kama nilivyosema ni mtu wa karibu sana. Sasa kwenda naye kuogelea kwangu sioni kama ni tatizo, ijulikane tu Aya ni mtu wangu wa karibu.” Alimaliza Idris.

Idris aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema ambapo uhusiano wao ulizidi kuwa maarufu ilipokuja kujulikana kwamba Wema amenasa ujauzito ambao ulidumu kwa wiki kadhaa na kutoka kwa bahati mbaya. Hata hivyo, uhusiano wao ulikuja kuvunjika huku sababu za kuachana zikifi chwa.

GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.