Hizi Hapa Sababu za Kukosa Usingizi Wakati wa Usiku - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hizi Hapa Sababu za Kukosa Usingizi Wakati wa Usiku

Tatizo la kukosa usingizi kwa kitalamu ni Insomnia ni tatizo endelevu linalosababisha mtu kushindwa kusinzia au kutodumu kwenye usingizi.

Kwa kukosa usingizi, mtu huyu kwa kawaida huamka hajihisi kuwa mpya , hali hii inasababisha kupunguza uwezo wa kufanya kazi wakati wa mchana.

Vitu vinavyopelekea kukosa usingizi ni :-

Msongo wa mawazo

Unaweza kulala kupita kiasi au kukosa usingizi kama una msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo hutokea pamoja na matatizo mengine ya kiakili.

Kukosa ratiba ya kulala

kukosa ratiba ya kulala kama kutokuwa na mda maalumu wa kulala, kazi za kuamsha mwili kabla ya kulala, mazingira yasiyo rafiki kwa ajili ya kulala, kutumia kitanda kwa kazi nyingine isipokuwa kulala ama kufanyia tendo la ndoa.

Madawa

Madawa mbalimbali yanaweza kusababisha hali ya kukosa usingizi kama vile madawa ya kupambana na sononeko, madawa ya moyo na shinikizo la damu, madawa ya aleji, viamsha mwili kama Ritalin na corticosteroid. Madawa mengi ya dukani kama madawa ya maumivu, mabawa ya kuzibua pua na kupunguza uzito na matumizi.

Kula sana wakati wa jioni

Kula chakula kidogo ni sawa, lakini kula kupita kiasi wakati wa jioni au usiku huweza kukusababisha hisia za kutohisi vyema kama ukilala chini na kusababisha kushindwa kusinzia.watu wengi pia hupata kiungulia, kubeua, ambavyo humkosesha usingizi.

Kahawa, nicotini na pombe

kahawa chai, cola na vinywaji vyenye virutubisho vya kahawa hujulikana kuwa ni viamsha mwili. Kunywa kahawa mchana au usiku huzuia mtu kupata usingizi usiku. Nicotine iliyo kwenye tumbaku na sigara huwa ni kiamsha mwili kingine kinachosababisha kukosa usingizi. Pombe hulegeza mwili na huweza kusababisha kusinzia lakini huzuia kufikia kilele cha usingizi na kwa kawaida husababisha kuamka wakati wa usiku.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.