Haya ni Mambo 10 Usiyoyajua Kuhusu Rayvanny wa WCB - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Haya ni Mambo 10 Usiyoyajua Kuhusu Rayvanny wa WCB

Rayvanny ni muimbaji wa pili kusainiwa na label ya Diamond Platnumz, WCB baada ya Harmonize kutoka. Baada ya hapo amelitangaza jina lake kwa kuachia kazi nzuri zilizomfanya kujikusanyia mashabiki lukuki.
Kutokana na uzito wa jina lake kwa mara ya kwanza kupitia Music Facts ya Bongo5 tunakuleta mambo 10 ya kawaida kuhusu Rayvanny lakini si rahisi kuyafahamu.

1. Mpenzi wake Rayvanny, Fahyma ambaye amezaa naye mtoto mmoja ametokea katika video tatu za msanii huyo. Kwa mara ya kwanza alionekana katika video ya Kwetu ambayo ni ngoma yake ya kwanza ya Rayvanny ndani ya WCB, video ya pili ni Natafuta Kiki na tatu ni Safari aliyomshirikisha na Nikki wa Pili.

2. Licha ya kuwa muimbaji mwanzoni Rayvanny alikuwa akirap, kitu hicho kimemfanya kushirikishwa na marapa wakubwa kama Fid Q na Chindo Man. Ila cha kukumbuka ni kwamba Chindo Man alimshirikisha Fid Q katika ngoma yake iitwayo Tofarati ya Mtaa.

3. Ngoma ya Rayvanny iliyopata views zaidi ya Milioni 10 katika mtandao wa YouTube ni Kwetu, ngoma hii ina views Milioni 11.2, nyingine zote zilizobaki zina views chini ya Milioni 10.

4. Ni msanii wa pili kutoka WCB kuchaguliwa kuwania tuzo za BET baada ya Diamond Platnumz lakini ni msanii wa kwanza ndani ya label hiyo na Bongo kiujumla kushinda tuzo hiyo. Mwaka jana alishinda BET kupitia kipengele cha Viewer’s Choice Best New International Act.

5. Queen Darleen ndio msanii pekee wa kike aliweza kumshirikisha Rayvanny katika ngoma yake tangu msanii huyo kujiunga WCB. Mwanadada huyo alimshirikisha Rayvanny katika ngoma yake inayokwenda kwa jina la Kijuso.

6. Jason Derulo ni miongoni mwa waimbaji kutoka nje ya Tanzania waliomshirikisha Rayvanny katika ngoma zao, Derulo alimshirikisha muimbaji huyo katika remix ya ngoma ‘Tip Toe’. Awali Ray aliweza kushirkishwa na Bahati kutoka Kenya na Safi Madiba kutoka Rwanda.

7. Ngoma ya Dogo Janja ‘Ngarenaro’ ndio ngoma ya kwanza kufanyika katika studio ya Rayvanny inayokwenda kwa jina la Surprise Music, producer wa studio hiyo ni Rash Don.

8. Licha ya kushinda tuzo ya BET zinazotolewa Marekani, hakuna taarifa zinazoeleza iwapo Rayvanny amewahi kushinda tuzo yoyote Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

9. Baada Q Boy Msafi kuonekana katika video ya Rayvanny ‘Natafuta Kiki’ iliyotoka August 2016, miezi miwili mbele baada ya hapo alimshirikisha Ray katika wimbo wake ‘Mugacherere’ ambao walifanya pamoja na Shetta.

10. Rayvanny ndiye msanii pekee wa WCB kufanya/kukutana na Diamond katika ngoma tatu, mwanzo alishirikishwa na Diamond katika ngoma ‘Salome’, wakakutana katika ngoma ‘Zilipendwa’ iliyokutanisha wasanii wote wa WCB, na mwisho ni katika remix ya ngoma ya Fid Q ‘Fresh’.

Wasanii wengine wa WCB waliobaki wamefanya/kukutana na Diamond katika ngoma mbili na wengine moja tu kama Lava Lava, Queen Darleen na Mbosso.

- Bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.