Davido: Sichepuki Ila Napenda Kuangalia Wanawake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Davido: Sichepuki Ila Napenda Kuangalia Wanawake

Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria, Davido amesema kuwa ni moja ya wanaume ambao huwa wanavutiwa kuangalia maumbo na uzuri wa wanawake lakini cha ajabu hajawahi kumsaliti mchumba wake Chioma.

Davido kupitia ukurasa wake wa Snapchat amethibitisha hilo kwa kusema kuwa huwa anapenda sana kuangalia wanawake hususani maumbo yao lakini cha ajabu hajawahi kumsaliti Girlfriend wake.

“Sijawahi kuchepuka ila napenda kuangalia kila sketi (Mwanamke) inayopita mbele yangu, Mimi sio mwanaume msaliti napenda sana kufanya mapenzi na Chioma,“ ameandika Davido kwenye ukurasa wake wa SnapChat.

Ijumaa ya wiki iliyopita mchumba wake na Davido, Chioma aliandamwa na skendo mitandaoni nchini Nigeria kuwa anamsaliti Davido.

Hata hivyo Davido siku hiyo hiyo ya Ijumaa baada ya kuzagaa kwa skendo za kusalitiwa na Chioma aliposti picha akiwa naye kitandani kuudhihirishia umma kuwa hajali maneno ya walimwengu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.