Casto Dickson: “Sijali Kuhusu Tunda Kuwa na Skendo na Wanaume Wengi Nampenda Ivo Ivo” - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Casto Dickson: “Sijali Kuhusu Tunda Kuwa na Skendo na Wanaume Wengi Nampenda Ivo Ivo”

Mtangazaji wa kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds Tv, Casto Dickson amefunguka kuhusu skendo zilizokuwa zinaendelea kwenye mitandao ya kijamii zilizo muhusisha mpenzi wake video vixen Tunda Sebastian

Casto Dickson na Tunda waliweka wazi Mahusiano yao siku chache zilizopita Lakini pamoja na kuwa mapenzi yao ni mapya lakini mambo ya zamani ambayo hawawezi kuyaepuka.

Mwanzoni mwa mwaka huu Tunda alikumbwa na skendo ya kuwa kwenye Mahusiano na staa wa muziki Diamond Platnumz na hata kusemekana ana ujauzito wake lakini pia alikuwa Kwenye Mahusiano na mfanyabiashara Kinje ambaye ni mume wa mtu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo5, Casto amemtetea mpenzi wake na kusema hajali Tunda alifanya nini au alitembea na nani kabla hajawa naye kwani walivyokutana waneanza upya:

"Mimi nimempenda Tunda kama Tunda naanzia naye pale nilipokutana naye kwenda mbele atakaponikosea kuanzia pale nilipoanza naye nikamkuta na mwanaume mwingine hapo ndipo ninapotakiwa kuanza kukasirika ila yaliyopita yamepita kwa sababu ni mwanamke na mimi ni mwanaume na mimi nimefanya mambo mengi huko nyuma kwaiyo sisi tunaanzia tulikokutana tunaendelea mbele tunamuomba Mungu atufikishe huko tunakoenda"

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.