Breaking News: Mwili wa Mmiliki wa Mabasi ya Super Sami Waokotwa Mtoni Kwenye Kiroba - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Breaking News: Mwili wa Mmiliki wa Mabasi ya Super Sami Waokotwa Mtoni Kwenye Kiroba

Mwili wa Mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah umekutwa katika mto Ndabaka eneo la Bunda /Lamadi

Taarifa kutoka vyanzo vya habari zinasema kwamba mwili wa Samson Josiah umeokotwa na wavuvi wa samaki jana jioni Jumatano Machi 14,2018.

Watu wa karibu na marehemu wanasema mwili uliookotwa ni wa Samson Josiah.

Miongoni mwa habari zilizoteka vyombo vya habari Tanzania tangu Machi 9, 2018 hadi ni kuhusu kupotea kwa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah kwa zaidi ya wiki mbili sasa. 


Mapema ilielezwa kuwa gari yake ndogo aliyokuwa akiitumia aina ya Toyota LandCruiser ilikutwa imechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyoko mkoani Mara siku ya Machi 9, lakini yeye mwenyewe alikuwa hajapatikana.

Kwa mujibu wa familia ya Bwana Josiah, ambayo inaishi mkoani Mwanza, ilidai kuwa siku ya kupotea kwa Josiah ambayo ni February 27, majira ya usiku, Josiah alimpigia simu mkewe na kumwambia kuwa atarudi nyumbani na mgeni, na hayo yakawa mawasiliano yao ya mwisho.

Mabasi ya Super Sami yanafanya safari zake kuanzia mkoa wa Mwanza, kwenda mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa pamoja na Kagera.

Chanzo: Muafrika Halisi blog & JF 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.