Amber Lulu: Simpendi Baba Yangu Hata Kidogo Na Wala Sitaki Kumuona - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Amber Lulu: Simpendi Baba Yangu Hata Kidogo Na Wala Sitaki Kumuona

Video vixen maarufu aliyegeukia sanaa ya Bongo fleva Amber Lulu amekiri kuwa amemtosa Baba yake mzazi na hataki hata kumuona.

Amber Lulu amefunguka hayo wakati anaelezea changamoto alizozipitia katika maisha yake baada ya Baba yake mzazi kuwakimbia na kumuacha yeye kama mtu pekee ambaye alitakiwa kuiangalia familia yake hasa mama yake ambaye alikuwa mgonjwa.

Amber Lulu ameongelea uhusiano aliokuwa nao na Baba yake mzazi ambapo amekiri katika umri mdogo alianza kushika majukumu mazito ya kuielea familia yake hivyo ilimbidi ajiingize katika biashara mbali mbali ili aweze kupata pesa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Amber Lulu aliongea haya kuhusiana na changamoto alizozipitia:

"Kipindi hiko nilikuwa bado niko shule lakini ilikuwa likizo hata ya wiki mbili nilikuwa nakuja Dar kufanya kazi maana tulikuwa tunahitaji pesa na mama Yangu alikuwa mgonjwa na ndio baba alikuwa kashatukimbia, nakumbuka msanii alikuwa anaitwa Pasha alinitumia kwenye video yake akanilipa shilingi elfu hamsini ambayo sikutumia hata senti nikaenda kumpa Mama yangu ambaye alikuwa anahitaji lakin moja na nusu ya matibabu”.


Lakini Pia Amber Lulu ameongelea uhusiano wake na Baba yake mzazi ambaye alimkimbia:

"Wanasema mzazi ni mzazi lakini mimi Baba yangu alinitelekeza kaja kunitafuta nilivyotoa wimbo wangu wa Watakoma alafu ananiomba hela kusema kweli aliniumiza kwa sababu hajanitafuta kama miaka kumi halafu anakuja kunitafuta kwa sababu anataka hela , dah kusema ukweli simpendi baba yangu hata kidogo na sitaki hata kumuona”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.