Lulu Diva – Siishi Mjini Kwa Kudanga Maisha Yangu Mazuri Kitambo - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lulu Diva – Siishi Mjini Kwa Kudanga Maisha Yangu Mazuri Kitambo

Mwanamuziki wa Bongo fleva aliyegeukia miondoko ya mduara Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi haishi mjini kwa kudanga kama watu wengi wanavyomzushia bali anapiga kazi na mpenzi wake ni mwanaume wa kawaida.

Siku za hivi karibuni Kumekuwa na maneno mengi sana ambayo yamesemwa kuhusiana Lulu Diva ambapo inasemekana kuwa malo zote alizokuwa nazo ambazo ni gari aina ya Prado na nyumba ya kifahari anayoishi Mbezi Beach vyote amepangishiwa na lake.

Kwenye Interview aliyofanya na Times Fm Lulu Diva amekataa habari hizo na kudai kuwa maisha yake ni mazuri kabla hata hajawa Mwanamuziki:

"Kwanza kabisa mimi maisha yangu ninayoishi na jinsi ambavyo nipo ni toka sijawa mwanamuziki nilikuwa na maisha haya sema mimi ni msichana ambaye nimehangaika sana nimeshafanya kazi hotelini nikawa waiter na biashara zote nimefanya kwaiyo nimehangika sana pesa yangu kwaiyo sijawahi kudanga hata siku moja Maisha Yangu mazuri ninayoishi nimeyafanyia kazi wala sijawahi kudanga"

Lulu Diva pia ameikana stori ya kwamba anachukuliwa kimapenzi na pedeshee ambalo linamuweka mjini na ndio linalompa kila kitu bali amedai mwanaume ambaye ni mpenzi wake ana maisha ya kawaida sana hana utajiri wa kiivyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.