Wanawake ni Chanzo cha Uovu Duniani, Muhubiri Asema - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wanawake ni Chanzo cha Uovu Duniani, Muhubiri Asema

Muhubiri wa kanisa la Seventh Day Adventist nchini Rwanda, Nicolas Niyibikora huenda akajikuta mikononi mwa polisi mara baada ya kudai kuwa wanawake ndio chanzo cha maovu ulimwenguni.

Kupitia mahubiri Yake yaliyorushwa na kituo cha redio cha Amazing Grace, Niyibikora aliwambia wanawake kwamba hawapendwi na Mungu na kuonya kuwa hakuna lolote jema linaloweza kupatikana kutoka kwao.

Kutokana na mahubiri hayo kukasirisha wengi kanisa la Seventh Day limefanya juhudi za kujitenga na Niyibikora ambaye wanadai aliipigwa marufuku kwa miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa gazeti la New Times tayari mahubiri hayo yamewakasirisha wanaharakati huku wale wanaounga mkono usawa wa kijinsia wakiitisha mkutano na vyombo vya habari na kuonya kuwa maneneo kama hayo yanaweza kusababisha chuki na mzozo miongoni mwa raia wa Rwanda iwapo hakuna hatua ya haraka itachukuliwa.

Source: BBC

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.