Wabongo Wampongeza Zari kwa Maamuzi ya Kuachana na Diamond - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wabongo Wampongeza Zari kwa Maamuzi ya Kuachana na Diamond

Baada ya Zari kutangaza rasmi kuwa kwa sasa hayupo tena kwenye mahusiano na mzazi mwenzie, Diamond Platnumz imeonekana hatua hiyo kupokelewa kwa mtazamo chanya na baadhi ya mashabiki wa Diamond Platnumz hususani wanawake.
Watu wengi ambao walikuwa wanawafuatilia wawili hao wameonekana wakitoa maoni ya kumpongeza kwa maamuzi aliyoyachukua ya kumuacha Diamond Platnumz.
Baadhi ya maoni ambayo yametolewa kwenye posti ya Zari kwenye mtandao wa Instagram, yamempongeza Zari kwa kumwambia kuwa yeye ni mwanamke jasiri na anayejitambua.
Hata hivyo sio mashabiki wote wamempongeza Zari wapo baadhi yao wamemkosoa kwa maamuzi hayo kwa kumwambia kuwa amekurupuka na amefanya maamuzi kwa hasira.
Jana Februari 14, 2018 usiku Zari kupitia ukurasa wake wa Instagram alitangaza kuwa hayupo tena kwenye mahusiano na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye amezaa naye watoto wawili.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.