Video: Diamond Rapa Aibuka Kutoka Nchini Kenya, Huyu Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Video: Diamond Rapa Aibuka Kutoka Nchini Kenya, Huyu Hapa

Baada ya kuwepo kwa mtu aliyedai kufanana na msanii wa muziki kutoka lebo ya WCB Wasafi, Harmonize na kujiita Harmo Rapa, sasa amekuja mwingine ambaye naye anadai kufanana na msanii mwingine kutoka katika kundi hilo hilo.

Mtu huyo ambaye ni dereva wa boda boda eneo la Mtwapa, Kaunti ya Kilifi, nchini Kenya anajulikana kwa jina Patrick Gongo Mabeya ameshika vichwa vya habari nchini humo kutokana na watu wengi kumfananisha na msanii Diamond Platinumz.

Kutokana na mfanano huo, Patrick amejikuta akila shavu la kufanya kazi na kampuni ya Car & General ya nchini humo.

Vile vile Patrick ameweza kujipatia shavu jingine la kuwa balozi wa pikipiki aina ya TVS kwa mwaka mmoja nchini humo na kupewa pikipiki mbili.
Patrick aliyevaa Tshirt Nyekundu akiwa na Erick Omondi pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya pikipiki za TVS wakati akikabidhiwa pikipiki hizo.

Mambo yalizidi kung’ara kwa Patrick pale ambapo alikutana na mchekeshaji maarufu nchini humo, Erick Omondi ambaye mbali na kucheza na mabvu za watu katika majukwaa mbalimbali ndani na nje ya Kenya, pia huwa anafanya kipindi kinachoitwa “How to Be” ambacho hukirusha katika chaneli ya Youtube.

Vilevile Erick Omondi amekuwa akirudia nyimbo pamoja na filamu mbalimbali za wasanii mbalimbali kwa lengo la kuwachekesha na kuwafurahisha madhabiki wake.

“Nilikutana nae Kaunti ya Kilifi miezi miwili iliyopita, kupitia rafiki yangu ambaye nilikuja kwenye harusi. Muonekano wake ambao unakaribiana sana na muonekano wa Diamond uliiteka akili yangu na mara moja nikamtaka anisaidie katika kufanya stori ya maisha ya Diamond,” aliandika Erick.

Itazame hapa Video ya A Boy From Tandale aliyoifanya Erick Omondi kwa kushirikiana na Patrick (Diamond Rapa)

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.