Tunda Awekwa Kitimoto na Familia Yake Kisa Video Akiwa Kwenye Mahaba Mazito Kusambaa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Tunda Awekwa Kitimoto na Familia Yake Kisa Video Akiwa Kwenye Mahaba Mazito Kusambaa

Tunda Awekwa Kitimoto na Familia Yake Kisa Video Yake na Kinje Wakiwa Kwenye Mahaba Mazito Kusambaa
Kufuatia sakata la video akiwa anafanya vitendo vya kimahaba na mume wa mtu, Kinjekitile Kingunge ‘Kinje’ kusambaa mitandaoni hivi karibuni, muuza sura katika video mbalimbali za wasanii wa muziki Bongo, Tunda Sebastian amejikuta akiwekwa kitimoto na familia yake.

Uchunguzi wa gazeti hili kupitia kwa rafiki wa karibu na Tunda ulionesha kwamba baada ya video hiyo kusambaa ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kwani wazazi wake walikasirishwa mno na kitendo hicho, ndipo wakamweka kitimoto japokuwa hadi sasa hajakaa nao sawa.

“Familia ya Tunda ilimweka kitimoto mwanadada huyo na kumsema sana ambapo aliahidi kwamba atabadilika na akawaangukia wazazi wake na kuwaomba msamaha licha ya kuwa haikuwa kazi rahisi kwa kweli,” alisema rafiki huyo.

Ijumaa Wikienda lilimtafuta Tunda ambaye alieleza kuwa, baada ya video hiyo kuvuja kulitokea mtafaruku mkubwa kwa wazazi wake huku mpenzi wake akikasirishwa na kitendo hicho na hadi sasa hazungumzi naye.

“Nimejifunza sana maana ile video imenivuruga sana kwa kweli kwani wazazi wangu walikasirika sana, mpenzi wangu mpaka sasa haongei na mimi ila bado ninaendelea kumwelewesha kwamba ile ilikuwa ni pombe tu.

“Naamini hasira zake zikiisha atanitafuta tu maana najua ananipenda, nimekoma kunywa pombe na nimeshaacha kabisa kwa kweli,” alisema Tunda.

Video hizo zilikuwa gumzo mitandaoni kabla ya Kinje kufiwa na baba yake, Mzee Kingunge hivyo watu kuacha suala hilo kwani ni kumuongezea maumivu juu ya maumivu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.