Tambwe Afunguka "Okwi Hamuwezi Chirwa" - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Tambwe Afunguka "Okwi Hamuwezi Chirwa"

Emmanuel Okwi
Mchezaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe, amewachambua Obrey Chirwa wa Yanga na Emmanuel Okwi wa Simba halafu akasema Okwi hamuwezi Chirwa na ndiye atakayekuwa mfungaji bora msimu huu.

Okwi ambaye kwa sasa anaongoza kwa ufungaji kwenye Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 14, amemzidi Chirwa anayeshika nafasi ya pili kwa ufungaji akiwa na mabao 11.

Tambwe ambaye msimu huu amekuwa na majeraha ya mara kwa mara, ameshindwa kuitumikia ipasavyo timu yake na kujikuta akishindwa kufunga hata bao moja katika mechi chache za ligi alizocheza.
Obrey Chirwa wa Yanga
Akizungumza na Championi Jumamosi, Tambwe alisema: “Binafsi naona Okwi hamuwezi Chirwa na (Chirwa) ndiye atakayekuwa mfungaji bora na siyo Okwi, kutokana na rekodi zao zilivyo.

“Ukiangalia mabao ya Okwi na Chirwa katika ligi, yanatofautiana sana, Okwi amefunga sana sehemu moja ambapo ni Dar es Salaam tofauti na Chirwa ambaye uwanja wowote anafunga.

“Kutokana na hilo, naona Okwi hamuwezi Chirwa katika ufungaji,”
alisema Tambwe ambaye msimu uliopita alifunga mabao 12.


Akizungumzia kauli hiyo ya Tambwe, Chirwa raia wa Zambia, alisema anaamini atampita mpinzani wake huyo na kuongeza kuwa, hivi sasa anaona ni kama ametangulia tu na haiwezi vita ya kuwania tuzo hiyo ya ufungaji bora.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.