Steve Neyerere: Sura za Bongo Movie Zinachosha - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Steve Neyerere: Sura za Bongo Movie Zinachosha

Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ anaamini kuwa, soko la sinema za Kibongo haliwezi kubadilika kama sura za waigizaji ni zilezile za kila siku ambazo hata yeye amezichoka.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Steve alisema kuwa, kama kila mtu anapotazama sinema anakutana na sura ya Kajala Masanja, Shamsa Ford, Aunt Ezekiel na wengine, watu wanachoka na mwisho wa siku ndipo linatokea anguko la sinema kama lilivyotokea.

Steve alisema kuwa, inatakiwa ufike wakati wale mastaa wakubwa waachie ngazi na kuwapa nafasi wengine ili watu waone ladha tofauti maana sura zao zimechosha mashabiki.

“Ninachokipigania ni kwamba waigizaji wakubwa wabaki na haki miliki zao, lakini sura za mastaa hao hao zinachosha maana hata mimi nimezichoka,” alisema Steve.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.