Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 6 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 6

Riwaya: SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA.
Mwandishi: SEID BIN SALIM
SEHEMU YA 06
Ilipoishia......
Waliendelea kuongea taratibu huku wakiangalia newz mbali mbali kwenye mablogz na website.
" Duh huyu kaka ana sura mbaya kama usiku. Alisema maryam baada ya kuiona picha mbovu ya mtu.
" Anafaa kuwa mmeo huyu!.
" Loh!, ntampitisha wapi mimi huyu muone mdomo wake.
Alisema kisha akaachia kicheko, lucky alitabasam, hiyo ndo ilikuwa cheka yake sana sana pindi anapofurahi. alitoka kitandani akamwachia maryam laptop akaingia bafuni kwa ajili ya kuoga, ilikuwa inakimbilia majira ya saa sita kasorobo, kitendo cha lucky kuingia bafuni kiliwafanya wakina amina wainuke vitandani kwao kuongea na Maryam.
Songa nayo......
" kumbe na wewe mnafiki hivyo ee!!. Alisema amina.
" kwa nini?.
" tuliahidianaje kuhusu weekend ya leo?.
" kwenda club night.
" So!. Alidakia tunu.
" Um jaman!, kwani hakuna jambo unaloweza kupanga kufanya kisha ukalighairisha?.
" Kwa iyo ushaghairisha.
" Ndio.
" kwa sababu ya huyu mshamba mshamba.
" Nisikilizeni nyie viumbe, kila mtu ana maisha yake humu ndani, msimwite mtu mshamba hali ya kuwa hamjui anasumbuliwa na nini!, nna iman lucky si mshamba wala sii wa kuja kama tunavyomdhania, kama nyie hamko tayari kubadilisha nia yenu ya kumnyanyapaa, mimi ntakula nae sahani moja na naitaji kumsaidia kuhakikisha anarudi katika hali yake ya kawaida. Ntatoka nae leo kwa kuwa amenikubalia, nyie tokeni tu mi siko pamoja nanyi leo. Alisema maryam.
" Leo hiyo we ni wa kuzungumza hivyo. Aliuliza amina.
" yah, lucky ni rafiki yangu, na ntafanya juu chini, hata pesa ntatumia ili siku moja nijue kitu gani kinamfanya akose raha.
" Sawa jitahidi. Alisema tunu.
" Mkishuka chini mtasikia story zake alichokifanya ndo mtajua kama ni mshamba au sii mshamba. Alisema maryam.
Lucky alitoka bafuni akiwa ametakata usoni, hawakuendelea kuongea wakakaa kimya, lucky alijipangusa akajiweka vizuri mwili wake akavaa nguo za kawaida alizozoea, maryam nae alivaa wakajiweka sawa kwa ajili ya kuondoka, kabla ya kutoka lucky aliwauliza wakina amina kama hawana safari yoyote kwa weekend hiyo ili ikiwezekana watoke wote, ila walikuwa wazito kumjibu maryam akamuitaji aachane nao wasepe zao..
Walipokuwa wanashuka ngazi kuelekea chini, maryam alitoa paswed cm yake ya iphon akaandika ujumbe mfupi ulioonekana kwenda kwa Sophia msimamizi wa wanafunzi wa chuo kiranja.
** Sophy, natoka na Lucky, nimefanya hivi ili kumbadilisha mazingira niangalie itakuwaje, naomba tushirikiane kumshawishi awe na furaha sii unaona yeye pekee ndo mwenye hali ya unyonge chuoni hapa?.
Kabla ya kuituma kuna cm iliingia, alifurahi baada ya kuona jina la mdogo wake wa mwisho, alipokea akaweka sikioni.
" Hellow my lovely sista.
" hellow too Shikamoo sista.. Sauti ya upande wa pili.
" Marhabaa how are you.
" Im cool and you.
" im okey umenikumbuka?.
" yah dada nimekukumbuka.
" uko nyumbani?.
" ndio nimekaa na mama.
" wow!, nakuja muda si mrefu nimewamiss sana, mwambie mum aongee na witty waandae chakula kizuri nakuja na rafiki yangu.
" Ok sista ntamwambia.
Cm ilikatika akaisend message kuelekea kwa sophia.
" Nyumbani ni wapi?. Aliuliza lucky.
" Ni mbezi beach samaki.
" kumbe mbali hivyo.
" No bhna. Tunachukua tax fasta tu hapo.
" unachezea pesa hivyo, kwa nini tusipande dala dala tukatumia elfu moja badala ya elfu 20.
" jasho la watu huwa sipendi.
Alisema maryam lucky akawa amefikiria kitu moyoni mwake na kuachia tabasam, walitoka hadi kwenye kituo cha tax wakachukua tax na kuanza safari, lucky mkononi alishikilia cm kubwa ya sony, maryam alikuwa na iphon ambayo aliitach kila wakati kutokana na message zinazoingia, alikuwa anapenda sana kuchart kuliko maelezo, moja ya watu aliokuwa anachart nao ni sophy ambao walikuwa wanachart kuhusu lucky kuweza kumrudisha katika hali yake ya kawaida, baada ya kugundua uenda kuna kitu kwenye maisha yake kimemuharibu kisaikologia kwa jinsi walivyomuangalia kwa haraka haraka hasa kwa tukio zito aliloweza kulifanya...
Walifanikiwa kufika mbez beach samaki kwenye mishale ya saa saba na nusu, familia nzima ya maryam ilikuwa nyumbani isipokuwa baba yake, waliingia ndani wakapokelewa kwa furaha za hali ya juu, Chakula kilikuwa tayari ikabidi kabla hata ya kupumzika wapate msosi, walipomaliza wote walikusanyika sebleni kupiga story, Maryam alitumia muda huo kumtambulisha lucky kwa mama yake pamoja na wadogo zake wawili waliokuwepo.
" Mama huyu anaitwa Lucky, ni mwanafunzi mwenzangu chuoni, tunakaa chumba kimoja, chake ni changu changu ni chake. and lucky huyu ndo mam wangu, hawa ni wadogo zangu na huyu Witty ni dada yangu yuko hapa kwa ajili ya kusaidia kazi si unajua.
" Yah!, nimefurahi kuwafahamu wote.
" Mimi pia nimefurahi sana kukufahamu binti.
" Asante. Alisema Lucky.
" Hatujaja hapa kukaa sana, nimekuja kuwaona tu na kuondoka sababu kuna sehemu tunaenda, Sauda.. Alisema maryam kisha akamuita sauda mdogo wake wa mwisho.
" Abee.
" Nenda kwenye meza ya chakula ukachukue mfuko nlokuja nao kuna zawadi yako na ya Farhat mule ndani.
" Sawa ila vibaya hivyo dada ina maana mnaondoka muda huu?.
" Yah.
" Nimekumiss dadaangu nataka kukaa na wewe.
" Usijali weekend ijayo ntakuja kushinda nyumbani.
" kweli?.
" Bhna kachukue huo mfuko usinitie wazimu. Sauda aliinuka akaenda kuchukua mfuko alioambiwa kwenye meza ya chakula.
" Baba na leo kaenda kazini?. Aliuliza maryam.
" Hapana kuna sehemu tu kenda. Si unajua baba yako asivyoisha mihangaiko.
" Mh! Aya sawa.
" Binti mbona umekaa kimya sana. Mama maryam alimuuliza lucky.
" Hapana kawaida tu mama usijali.
" Alafu mbona kama nliwahi kukuona sehemu au nimekufananisha?
" mimi?
" Yah.
" Labda. Siwezi kukataa wakati sijui wapi.
" Wee ni mtoto wa mzee Edwad yule mwenye kampuni ya magari kariakoo kwa wahindi au sie?. Aliuliza mama maryam swali lililomfanya lucky ajiulize maswali mia kidogo yasiyokuwa na majibu, mzee huyo kweli ndo alikuwa baba yake mzazi, ilibidi ajiulize amemjuaje na aliwahi kumuona wapi.
" mzee edwad hapana. Aliamua kukataa kutokana na kusikojua wala kukumbuka alimuona wapi, isije kuwa alimuona sehemu za uchafu uchafu katika enzi zake then akakubali tu heshima ikapungua.
" Ok samahani basi nlikuwa nimekufananisha. Maana yule mzee ana mtoto wake umefanana nae sana.
" Okey, itakuwa tumefanana tu duniani wawili wawili.
Maryam alikuwa anamuangalia mama yake kisha lucky jinsi anavyopokea maneno, kwa akili ya haraka haraka kuna kitu alikigundua machoni mwa lucky pindi alipoulizwa kuhusu mzee edwad, alihisi uenda ni kweli kwa jinsi lucky alivyolipokea jina la mzee huyo, ila hakutaka kuyaendeleza akaliweka moyoni ili siku nyingine aje ambane mama yake kuhusu huyo mzee..
Walitaniana na kucheka kama familia ndani ya lisaa limoja na nusu, furaha yao ilimtesa sana lucky aliekuwa anakumbuka maisha flan ya nyuma hasa baada ya kutajiwa jina mzee edwad, aliikumbuka familia yake ambayo hajaiona mwaka na zaid, hakujua lini ataiona, maryam aliingia chumbani kwake akachukua funguo za gari na kumuomba lucky waondoke, waliaga wakatoka nje na kuingia ndani ya gari.
Maryam alipoliwasha lucky alimuangalia kumbu kumbu za mawazo yake zikaenda mbali kidogo, akakumbuka baadhi ya vitu alivyokuwa anafanya kabla ya kuwa Lucky kama lucky, maryam hali ya lucky kuwa na mawazo aliiona, alimuita na kumuita tena lakini hakuitika, walipofika nje ya geti alimgusa begani akashtuka.
" Nini lucky?. Nini unawaza namna hiyo nakuita mara kumi kumi huitiki.?
" I'm Sorry maryam, nlikuwa mbali sana kimawazo.
" kitu gani ulikuwa unawaza.
" Soon utajua.
" Unanipa wakati mgumu ujue na sipendi unavyokuwa hivyo dia serious, Nkuombe kitu?.
" Yah.
" Naomba tupite kwenu tukasalimie pliz!. Alisema maryam kumtest lucky kisha akasikilizia atajibiwa nini.
" Siku nyingine usijali.
" Kwa nini isiwe leo?.
" Huwa napenda nkiongea na mtu mara anielewe.
" Ok poa.
Hakuitaji kwendelea na mada hiyo, aliamini mtu mwenyewe anaeongea nae kichwa chake nusu zimo nusu hazimo, walienda hadi msasani wakapita moja ya duka kubwa la nguo kufanya shoping ndogo, walipomaliza walienda moja kwa moja beach kuangalia mazingira na kuogelea pia.
" Napenda sana kuogelea sijui na wewe vipi?. Alisema maryam wakiwa ufukweni mwa bahari.
" Sii saana. Napenda tu kuyaona maji na kuyachezea chezea basi.
" poa, mi nakuacha hapa basi naingia kwenye maji japo dakika tano nikatoe mikosi.
" Usijali kuhusu hilo best.
Alivua nguo zake akabaki na nguo za ndani, alitoa kimtandio kwenye mkoba akajifunga kiunoni chengine kichwani, lucky alimwangalia bibie alivyo na mwili mzuri wa kuvutia, alimsifia maryam akaelekea zake kwenye maji, alipofika alijitupa akazamia ndani na kwenda hadi kwenye maji makubwa.

NINI KITAENDELEA KATIKA EPISODE YA 07 ? Kesho pita katika App yetu hii ili uweze kupata muendelezo  wa utamu wa stori hii. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.