Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 10 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 10

Riwaya: SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA..
Mwandishi: SEID BIN SALIM
SEHEMU YA 10
Ilipoishia......
" Aje afikishe aone kama sijamnyuka makwenzi.
" Mama yako nae je ashakuwa kizee ee!.
" Uzuri wote huo mamaangu, wee bado mbichi sana baba akikuacha leo ukaingia mtaani lazima uwapelekeshe, jicho jicho mdomo wa lips chezea!. Alisema akiachia tabasam lililomfanya mama acheke, walikuwa kama mtu na shost yake, kwa jinsi walivyokuwa wanaongea angeingia mtu akaambiwa ni mtu na mama yake isingekuwa rahisi kuamini.. Tuachane na hayo, nimekuja hapa na kitu kimoja mamaangu nataka unisaidie. Alisema baada ya kumaliza kucheka.
" Kitu gani?. Aliuliza ashura akikaa vizuri kwenye sofa kumsikiliza mwanae.
" Kuhusu mzee edwad uliemtaja jana nlipokuja hapa na rafiki yangu Lucky..

Songa nayo......

" Mh!, wee mtoto ushaanza mabalaa yako ee!. Aliuliza ashura.
" Mabalaa gani mama?.
" Sasa unamuulizia mzee wa watu ili iwaje?.
" Dah, kwa hiyo mama una maanisha namuuliza ili awe mwanaume wangu?.
" Sasa wa nini?.
" Mama uliza kwanza kabla hujaisi vibaya.
" Wa nini?. Hamchelewi watoto wa vyuo mara nlipokuambia ana maduka kariakoo akili yako hoi, na yule mzee sii mtu mzuri labda kama kaacha sasa hivi. Alisema ashura na kumuacha mwanae njia panda, alijiuliza sii mtu mzuri kivipi, kitu kilichomchanganya akilini mwake.
" Mamaangu hujanilea hivyo, kama ndivyo ulivyonifundisha haya. Alisema maryam baada ya kuwaza vitu kichwani mwake kuhusu maneno aliyoyaongea mama yake.
" Haya nambie wa nini?. Aliuliza ashura.
" Yule rafiki yangu nliekuja nae kuna matatizo anayo. Tokea aingie chuo hatumjui baba yake mama yake wala ndugu yake yoyote, ukimuuliza kuhusu baba anaweza kukupiga ngumi, na inaonekana ametokea sehemu moja ya maisha flan mazuri ila magumu yaliyomharibu kisaikologia, naomba unielekeze kwa huyo mzee kwa sababu ulipomsema mbele yake alishtuka akaonekana kubadilika.
" Sawa, yule mzee mimi nlimfahamu mwaka juzi, ni mtu maarufu sana africa mashariki kutokana na kazi anayoifanya, ila anaonekana kuwa mzee ambae hajatulia kiukweli, mkewe ni ndugu wa mama shakira hapo jirani nyumba ya tatu.
" Mama shakira yule mbunge na mwanasheria wa chama cha chadema?.
" Huyo huyo, nlikuwa karibu nae sana siku za nyuma kabla hajawa bize, kila siku lazima alinipatia malalamiko ya ndugu yake huyo kuhusu mmewe ili tusaidiane kumpa ushauri.
" unaifahamu kiundani kidogo hiyo familia?.
" Familia gani?.
" Ya mzee edwad?.
" Mimi namfahamu huyo mzee edwad na huyo ndugu wa mama shakira ambae ni mke wa huyo mzee.
" Anaitwa nani?.
" Jenipha. Anafanya kazi mhimbili ni mganga mkuu, kisha nlipoenda pale nlimkuta mkaka mmoja hivi nae ni mfanya biasha mkubwa wa kusafirisha madini ambae nliambiwa ni mtoto wao mkubwa, akitoka yeye anafata wa kike ila huyo wa kike sikuwahi kumuona, wako wawili tu.
" Mh!, mama naomba unielekeze niende uenda hii familia inamhusu huyu mwanadada.
" Masaki maduka mawili.
" Masaki maduka mawili?.
" Ndio, masaki mwisho kule tulipowahi kwenda kwa mwarabu wa dubai.
"Enhe nshapakumbuka.
" Pale kuna sehemu panaitwa maduka mawili, kuna maduka mawili moja la matunda lengine la vyakula, ukifika hapo tu na bahari unaiona, kuna nyumba nyeupe ya ghorofa mbili bati lekundu linang'aa ndo hiyo hiyo. Au ukifika hapo uliza kwa mzee edwad ni wapi? Utaoneshwa.
" Basi ngoja nsichelewe, nachukua gari dingi akija mwambie dogo kaondoka nalo.
" Atakuchinja shauri yako.
" Hawezi, watoto wake wote mimi ndo nimempa heshima ya kufika chuo, rais wa badae.
" Uwe rais wewe!.
" Haiwezeakani?.
" Machachari wewe.
" Hujui kama siasa lazima uwe mashauzi.?
" Yani hao watakao kupa urais itabidi wapelekwe mochwari watakuwa hawana akili. Alisema ashura kumwambia mwanae wakaachia kicheko, alimjua vizuri alivyo hivyo kumwambia hivyo hakukosea, japo alikuwa mtiifu mwenye huruma ila hakuwa ametulia kufaa kutumikia Taifa.
" Mwanangu wewe kwanza kazi za kuajiriwa zitakuwa kero kwako, wee soma tu elim ikubali uje uwe na kazi zako binafs basi.
" Na kweli mama, ngoja niende basi bayee. Alisema akainuka alipokuwa amekaa na kumsogelea mama yake, alimwachia busu akaenda chumbani kuchukua funguo ya gari, alipokuwa tayari anayo alipita seblen akaaga vya mwisho akaondoka zake, safari yake ilikuwa ni ya moja kwa moja masaki, huku akimuomba Mungu analolifata akute ndilo ili isije akaenda mkombo na kukwama.
Lucky nae njaa ilipomkamata alienda restaurant kula wakina amina wakiwa tayari wako room, alipomaliza alirudi ndani akajitupa kitandani akalala na cm mkononi, ile hali ya kulia kila anapokuwa kitandani haikuwepo tena, mwili kidogo ulichangamka mchango wa maryam ulianza kuonekana. deniss aliendelea kupatiwa matibabu katika chumba cha huduma.
Kipigo toka kwa lucky kilikuwa kikali kwake kilichompatia maumivu kila kona, alijiuliza mara kwa mara afanye nini ili amuombe lucky msamaha yaweze kuisha, alijilaumua nafsi yake kwa nini tamaa zake zimempeleka kubaya kusikostahili.
" Sikutegemea kwa uzuri wa yule mwanamke kama atanipatia majeraha haya?. Mwanamke anapiga utafiri anold haloo!. Ila nimekoma kuwashobokea madem nimekoma deniss nimekoma sirudii tena ng'o, sijui nimuingieje ili nimuombe msamaha, ila kwa namna alivyo kila akiniona kabla hata sijaomba msamaha ananitwanga itawezekana kweli?. Hapana..... alijisemea moyoni mwake.
kwa picha aliyovuta aliona sii rahisi na ataendelea kuchezea kipigo kila atapoonekana nae, kibaya zaid tayari watu waliokuwa wanamueshimu hasa watoto wa kike walishamdharau kwa kipondo alichopatiwa bila hata kujitetea.
" Yani sasa hivi sijui kama kuna mwanamke ntamtongoza hapa chuoni anikubalie, heshima yangu imeisha deniss dah.
Aliamini heshima yake imepungua na itaendelea kupungua kila leo chuoni bora afanye utaratibu awasiliane na wazazi wake wamfanyie uhamisho wa chuo aende chuo chengine.
Lucky akiwa chumbani kwake aliyakumbuka maneno aliyoambiwa na profesa, yalimrudia rudia mara kumi kumi kichwani akaona kitu alichoambiwa ni cha kweli, ili ndoto zake zitimie lazima akubali kulipita burungutu la kinyesi lililoko mbele yake, wapo watu walioandaliwa kuwa changamoto kwake kama deniss na ataendelea kukutana nao, ikiwa anataka kutimiza ndoto zake za kusoma anatakiwa awapite kushoto bila kujali wamefanya nini kwake ili yake yasonge mbele.
Aliinuka kitandani akatoa khanga aliyokuwa nayo mwilini na kuvaa nguo zake za kawaida, alijiangalia kwenye kioo kama yuko sawa, wakina amina kila mmoja alikuwa kitandani kwake ameweka mahedphon masikioni kwa ajili ya kula miziki mizito mizito, alipoona yuko sawa alichukua cm yake kitandani akavaa viatu vya simpo na kutoka nje, alienda hadi kwenye chumba ambacho deniss alikuwa anapatiwa matibabu akiwa yuko katika wakati mgumu wa kufikiria juu ya vipondo viwili alivyopewa ndani ya siku mbili dabo.
Madaktari walishangaa kumuona lucky anaingia kwenye vyumba hivyo, hawakuitaji kumuamini na kumuacha asogee sehemu alipo denis wakihisi uenda ameenda kulianzisha upya, walimzuia lakini akawaomba apite hajenda kishari, walimruhusu akasogea hadi sehemu alipo deniss nyuma yake akifatwa na watu wawili ili akilianzisha wamuwahi, hawakumuamini hata kidogo japo alishawaambia hayuko kishari.
Deniss alipomuona mwili wote ulikufa ganzi akaanza kutetemeka, alijua tayari balaa lishamfikia hadi hospitali akahisi haja kubwa kutaka kumtoka ghafla, kijasho kilimserebuka midomo ikapishana, lucky alifika akakaa kwenye kiti na kumwangalia, alipoona hali yake aliachia tabasam kisha akampatia pole iliyoonekana ya kinafiki.
" Unajisikiaje unapolazwa kwenye kitanda cha matibabu kwa ujinga wako wa kushoboka mwenyewe?. Usipende kuyaingilia maisha ya watu usiowafahamu kijana, sio kila tunda lililong'aa unaweza kulila likakuongezea afya mengine yashaoza ndani japo nje yanang'aa ukila tu mara unapoteza maisha, ukitoka hapa kamshukuru sana profesa kwa sababu ndo amefanikiwa kukuombea msamaha lakini ningekupatia vitasa mpaka hiki chuo ukihame, Bora ukorofishane na mvuta bangi mtumia madawa kuliko kukorofishana na mimi ambae sijawai kutumia hivyo vitu ila akili yangu ni zaid ya watu wanaotumia hivyo vitu. 
Najua ulinitamani kwa sababu mimi ni mtoto mzuri navutia, jicho jicho tako tako na nna vitu vyote vinavyomfanya mwanaume awe chizi, simaanishi wale wasiokuwa navyo hawampati mtu no, ila asilimia kubwa ya wanaume wanapenda mwanamke wa aina hiyo, kama ungenikuta katika enzi zangu ungenipata, ila sasa hivi umechelewa sana na baada ya kunipata ndo kama hivyo unaambulia kipigo, Sorry brother, lile bifu langu limeisha, ila popote utaponiona, nione kama dada yako au mwanaume mwenzako ambae ukinivulia nguo naweza kukutengeneza kama ambavyo mwanaume mwenzako ukimvulia nguo anavyokutengeneza. Good day and!, Samahani kwa maneno yangu kama nimekuboa, but lile bifu letu limeisha. Usimwone kila msichana mzuri unaweza kuupata mwili wake kuuchezea kwa jeuri ya pesa zako au cheo cha wazazi wako, ukiwa hivyo utaumia kwa sababu kuna wanawake wazuri zaid yangu na wao ni vichaa walivuta bangi kabla ya kutoka kwenye matumbo ya wazazi wao zaidi yangu.

NINI KITAENDELEA KATIKA EPISODE YA 11 ? Kesho pita kwenye App yetu kupata uhondo zaidi. Kama bado hauna App yetu >BOFYA HAPA< Kuipakua kwenye Simu yako.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.