Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 9 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 9

Riwaya: SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA..
Mwandishi: SEID BIN SALIM
SEHEMU YA 09
Ilipoishia......
" Haya ni maisha yangu binafsi, kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria itabidi wanaotaka kunichukulia hatua wajipange, kwa nini yeye isiwe kwa mwengine?. Kuna mtu yoyote nliwahi kumtukana au kumtolea maneno machafu why yeye, Profesa hamad nakueshim sana ila nadiriki kutamka mbele yako, Ama zake ama zangu, aondolewe yeye hapa chuoni au mimi, laa sivyo ntakula nae sahani moja kila ntapoonana nae hiyo ndo kazi, anayajua maisha yangu hadi anambie mimi nawategemea mabwana chuoni kusoma?. Nliwahi kumuomba hata shiling moja baada ya kupungukiwa, mbele ya pablic ya watu anaitaji kuniondolea heshima yangu nliyonayo chuoni nimfanyaje, mara ngapi nachukua tuzo za nidhamu ina maana gani, sina ina maana mwanafunzi mtiifu msafi na asiekuwa na tabia mbovu?, why anichokonoe?. I swea my professa mbele yako naapa popote ntapomuona Denis lazima nimtembezee kipigo, kwa kuwa nguvu ninazo uwezo ninao, atajua kuwa kuna wanawake vichaa walivuta bangi kabla ya kuzaliwa kwao sii wanaume tu.. alisema lucky kwa sauti ya kupanda na kushuka huku machozi yakimtoka kutokana na hasira alizokuwa nazo, hakujali maneno hayo anamuambia nani mbele ya umati wa watu ambao ulishakuwepo, Amina na tunu walikuwa katika mshangao mkubwa wa kujiuliza huyu ndo lucky ambae wanaishi nae chumbani kwao siku zote au sie?

Songa nayo......

" Ni nani rafiki wa huyu binti.? Aliuliza profesa alietambulika kwa jina la Hamad.
" Its me profesa. Alisema maryam.
" Mpeleke room akapumzike baada ya masaa mawili naomba umlete ofisini kwangu.
" Okey.
" Mpelekeni huyu kijana akapatiwe matibabu. Kisha aligeuka upande wa deniss akawaitaji watu wampeleke kwenye vyumba vya matibabu akatibiwe..
Maryam Alimchukua lucky akatoka nae eneo hilo, kila mmoja alikuwa haamini kilichotokea, wapo baadhi ya waliokuwepo katika tukio la mwanzo na kushuhudia hilo pia, Lucky alikuwa gumzo chuoni kwa karibia wanafunzi wote. Deniss alifanyiwa matibabu wakamuweka mabandeji usoni jichoni na kumfanyia huduma nyingine sehemu mbali mbali za mwili wake, huku maryam aliingia na lucky chumbani akafunga mlango, alimkalisha kitandani kisha nae kukaa pembeni, alimwangalia bila kummaliza akamuita..
" Lucky!.
Lucky aligeuka akamwangalia maryam bila kuitikia.
" Kwa nini unakuwa hivyo mpenzi wangu ee!, nionee mimi huruma basi mimi mbona nakuonea huruma lakini?. Alisema machozi yakimtoka. Em fikiria kila mmoja chuoni anakuchukuliaje sasa hivi, baada ya masaa mawili profesa hamad amesema twende ofisini kwake unajua kitu gani anakuitia?. Kama ni adhabu je anaitaji kukupatia. Aliendelea kusema kwa hisia.
" Niache kama nlivyo maryam, ntaishi nnavyopenda na sii wanavyopenda, hakuna anaejua matatizo yangu nliyonayo, hata ikitokea nkafukuzwa fresh tu hamna tabu, kusoma ntasoma hata mitaani lakini siwezi kuona nakosewa adabu na mpumbavu mmoja.
" Usiongee kwa utashi wa mdomo wako Lucky fikiria kwanza, kwa hiyo uko tayari kuniacha mimi hapa chuo urafiki wetu ufe kisa mambo hayo?.
" Akili zangu huwa ni mbili tu kichwani siku zote, nna akili ya kumueshim mama yangu, na akili ya kuwaza jambo lililopo sii linalokuja wala lililopita.
" Fine!, Okey Lucky, but remember i love you na nimekuzoea now siku mbili hizi, nna urafiki wa dhati kwako na siko tayari kuupoteza kwa kuona mwelekeo wako, nna imani ipo siku moja yatakwisha, siko okey ngoja niingie bafuni kujimwagia maji then twende ofisini kwa ticha au vipi?..
" Haina haja!, akili yangu inaniambia nitoke tu chuoni kwenyewe, nahisi maisha ya chuo yatanishinda so bora niachane na masomo niende kuishi maisha yangu ya kitaani. Alisema lucky.
" Eh!, kwani una nini lakini jamani lucky mbona hivyo?.
" Nakujoke ntabaki. Alisema lucky kumpoza maryam baada ya kuona maneno ya kuwa anataka atoke chuoni kwenyewe yamemuuma, lakini kichwani kwake kweli alishakuwa na mawazo ya kutoka chuoni kwani alihisi hakuna atachokifanya kikafanyika ikiwa akili zake zinazidi kuchanganywa kiasi hicho.
Waliongea maryam akaingia bafuni kujimwagia maji, lucky nae alivua nguo za class akavaa khanga nzito nakuingia bafuni baada ya maryam kutoka, walipomaliza wote waliongozana kuelekea kwenye ofisi ya profesa hamad kwenda kumsikiliza anasemaje.
" Lucky. Walipofika na kukaa kwenye viti vilivyokuwa mbele ya meza yake, walisalimiana baada ya salam profesa akamuita lucky.
" Naam.
" Akili yako iko sawa?.
" Yah iko sawa.
" Huna kitu chochote kinachokusumbua?.
" Yah sina.
" Why unafanya vitu vinavyopelekea kuondoa nidhamu yako uliyonayo kwa muda mrefu sasa hapa chuoni.?
" Nisamehe profesa ila sitoweza kukueleza chochote, zaid ya yote ntaomba msamaha lakini kujielezea kiukweli siwezi.
" Ok, nimetoka kukutetea katika uongozi wa juu, na kutokana na busara yangu nliyonayo nimeeleweka na umesameheka, nakuchukulia kama binti yangu nyumbani hasa kutokana na tabia nzuri unazozionesha, na mtoto akikosea kwa kawaida mkanye sii kumfukuza nyumbani, achana na watu piga kitabu, usimwangalie mtu anaitaji uishije, bali jiangalie mwenyewe unaishije ili uweze kufika mbali, mafanikio yako yako mikononi mwako japo kuna vizuizi vya watu wengi, mgomvi aliezoea kufanya ugomvi kumkorofisha mstaarabu ndo kazi yake, kuna watu wameumbwa kuharibu maisha ya watu na hawafurahi kuona mtu anaishi vile anavyotaka, wanapenda kuona anaishi vile wanavyotaka, wao wanataka wamuone hana furaha, maendeleo yake yanafeli, usiwaangalie hao wapite kushoto ili yako yaende. Sehemu ya kuingizia funguo katika kitasa cha mlango wako imechoka, badilisha kitasa au eneo la funguo ili wezi wasije kuiba mali zako okey!. Penye mafanikio lazima viwepo vikwazo, usizikatishe ndoto zako kwa sababu ya upumbavu wa mtu mmoja. Alisema profesa hamad akiwa anazunguka taratibu katika kiti chake kisha kumpiga fumbo dogo, ambalo haraka walijua maana yake halikuwa gumu sana kuleta maana.
" Okey asante kwa ushauri wako, ntaufanyia kazi na nisamehe sana.. alisema lucky.
Maneno aliyoyaongea bwana mkubwa yalimuingia vizuri kichwani, japo alikuwa na akili nusu lakini alipoambiwa kitu kizuri akili yake ilikishika, alimuelewa mr hamad na akawa tayari kuyafanyia kazi maneno aliyoambiwa, maryam nae alifurahi mno moyoni kwa maneno ya mr hamad, yalikuwa maneno mafupi lakini ya kuukonga moyo, alijua kweli huyo ni prifesa wa saikology hakuitwa profesa ili mradi profesa, aliamini lucky kwa maneno aliyoambiwa na jinsi yalivyoonesha kumuingia lazima yatasaidia kwa mara moja au nyingine, hakukuwa na lengine la ziada walitoka wakarudi room.
Walifika wakakutana na wakina amina tayari wakiwa wametoka class, maryam hakukaa alimwambia lucky anatoka anaenda nyumbani kwao kurudisha gari, lucky alimpa tano ya kishkaji maryam akaondoka zake kwenda mbez ya samaki, nia yake ilikuwa kwenda kumhoji mama yake juu ya mr edwad na sii kurudisha gari kama alivyomwambia lucky, alitaka kufatilia kwa gharama yoyote ili aujue undani wa lucky japo ilikuwa hatari kwake endapo lucky mwenyewe angejua.....
Amina na tunu mchana walitoka chumbani kwenda lunch.
" Rafiki yangu unaweza kuishi na mchawi usimjue hadi siku Mungu atapoamua kumkuonesha. Alisema Amina wakiwa wanashuka chini.
" Kwa nini?.
" Hivi lucky ulivyokuwa unamuona kalegea legea vile ulidhania anaweza kupigana na mtu kama deniss?.
" Hahahaaaaaaa!, mbona unanchekesha wewe?, Nlishasahau hasa tukio lenyewe, kwanza chanzo kilikuwa nini hadi kumbalaguza vile?.
" Maryam ndo wa kumuuliza swali hilo.
" na kweli atakuwa anajua, si unakumbuka maneno yake aliposema mkienda chini mtajua kama ni mshamba au sii mshamba?.
" Aaaahaaaaaaaaaa okey picha inanijia, inaonesha hili varangati ni la toka jana, ujue jana deniss nlionana nae jioni hivi, usoni kavimba vimba, mara anachechemea nkajiuliza vipi?. Alafu nkimsemesha mara anaogopa kujibu kuuuumbeeeee!!.
" Maryam akirudi atupe A to Z.
" unadhani atasema yule?.
" Kwa nini asiseme?. Namchamba kweli akileta mashauzi.
" Deniss nimemtoa hadhi kupigwa na mwanamke.
" Yani wee acha tu na atahama hiki chuo.
" Mwenyewe hapa nshaogopa kukaa kwenye hicho chumba siku anatuchenjia anatunyuka, nguvu zenyewe zilivyo mbili hivi!.
" Hhhhhm amnyuke nani?. Labda akunyuke wewe sio mimi namfungia mtaa chuo anakihama bila kutaka manina zake, anipige mie!, loh.. alisema Tunu.
" Utampiga na uembaba huo?. Mwili nyumba ule.
" Nataka uwe shamba nyumba ndogo lakini hanipigi, akinishinda nguvu mawe na meno haviuzwi..
Amina aliangua kicheko kwa alichokiongea rafiki yake, Walifika hotel wakaagiza chakula, waliendelea na story topic ikiwa ni kumuongelea lucky, jina lucky lilikuwa kwenye vinywa vya watu wengi sana chuoni, alikuwa maarufu kutokana na ukimya wake lakini sasa akawa maarufu kwa alichokifanya..
Saa nane maryam alifika mbez beach kwao akafunguliwa geti na kuingia ndani, alipaki gari akakutana na mdogo wake wakasalimiana, alikuwa na vijizawad akampatia wakaenda wote hadi seblen alikokutana na mama yake, alimsalimia akakaa chini wakafungua ukurasa wa maongezi.
" Jumaa tatu leo ulikuwa na kipindi asubuhi?. Aliuliza mama yake aliejulikana kwa jina la Ashura.
" yes!, tumemaliza mapema mno nkaona nirejee nyumbani vipi baba alipokuja hajaulizia gari?.
" Gari ni yako ataiuliziaje?.
" Weee hachelewi yule mzee, mwanafunzi yule ashaanza mambo ya starehe nimemnunulia ili ije imsaidie badae anaitumia sasa hivi mpumbavu yule ngoja aje!. Alisema akimuact baba yake anavyokuwa anaongea.
" Kwa hiyo baba yako ashakuwa mzee. Aliuliza ashura.
" Dingi eti yule uoni uso ushaanza kuisha, scrab tu ndo inamsaidia laa sivyo angekuwa kama nyani.
" Shauri yako kitinda mimba yupo hapa unamjua kwa kufijisha taarifa.. hajasema kitu aliulizia tu mbona gari moja haionekani nkasema kachukua mwenye nayo..
" Aje afikishe aone kama sijamnyuka makwenzi.
" Mama yako nae je ashakuwa kizee ee!.
" Uzuri wote huo mamaangu, wee bado mbichi sana baba akikuacha leo ukaingia mtaani lazima uwapelekeshe, jicho jicho mdomo wa lips chezea!. Alisema akiachia tabasam lililomfanya mama acheke, walikuwa kama mtu na shost yake, kwa jinsi walivyokuwa wanaongea angeingia mtu akaambiwa ni mtu na mama yake isingekuwa rahisi kuamini.. Tuachane na hayo, nimekuja hapa na kitu kimoja mamaangu nataka unisaidie. Alisema baada ya kumaliza kucheka.
" Kitu gani?. Aliuliza ashura akikaa vizuri kwenye sofa kumsikiliza mwanae.
" Kuhusu mzee edwad uliemtaja jana nlipokuja hapa na rafiki yangu Lucky.

NINI KITAENDELEA KATIKA EPISODE YA 10 ? Kesho pita kwenye App yetu hii kupata muendelezo wa uhondo huu. SHARE NA MARAFIKI WASOME PIA.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.