Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 8 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 8

Riwaya: SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA.
Mwandishi: SEID BIN SALIM
SEHEMU YA 08
Ilipoishia......
Hakuna kilichoendelea kwa usiku huo zaid ya usingizi, kipindi lucky anautafuta usingizi maryam yeye aliendelea kuwaza baadhi ya mambo aliyoyashuhudia kwa lucky.
" Kesho nkitoka class inabidi niende nyumbani kuongea na mama anambie kuhusu mzee edwad nimjue, uenda ndo mzazi wa Lucky.
Alijisemea moyoni mwake akavuta shuka kwa ajili ya kuanza kuutafuta usingizi, hadi kufika saa saba hakuna aliekuwa macho, Amina na tunu wao hawakuwepo, walikuwa wameenda sehemu za starehe kuisindikiza weekend, hawakuwa na mchezo na siku hiyo kwa kuwa nafasi yenyewe kuipata ni mara moja kwa wiki, siku nyingine zote wanakuwa bize na masomo..

Songa nayo......
Asubuhi na mapema wanafunzi wote wa chuo hicho kikuu dar es salam waliokuwa na vipindi asubuhi akiwemo maryam tayari walikuwa madarasani kuwasubiri walimu waje kuwapatia kile kilichowaweka chuo, hali ya hewa ilikuwa safi hasa maeneo hayo ya chuo, walipata nafasi ya kusoma vizuri kiubarid cha chini kikipenya madarasani. vipindi vilipoisha maryam ndo alikuwa wa kwanza kutoka akiwahi kwenda kufanya mambo yake mengine, kwa muda huo alikuwa anawaza sana kuhusu lucky kuliko hata masomo yake, hakuitaji kumtenga na kumnyanyapaa kutokana na alivyo kama walivyofanya wenzake, alitaka kufanya juu chini hata pesa kutumia kuhakikisha anajua kinachomsumbua na ikiwezekana amrudishe katika hali yake ya kawaida..
" Lazima nikupiganie Lucky my friend, nlikosea mwanzo nlipofurahi kuona huna furaha ila nimejifunza kutokana nawe na kuona kuna vitu vingi unavikosa. Nakupenda rafiki yangu. Alisema moyoni kipindi anatembea.
Akiwa katika mkusanyiko wa mawazo kuhusu lucky mwanadada alietokea kumuweka akilini kutokana na hali yake, alisikia sauti inamuita ikitokea nyuma iliyomfanya asimame ageuke kuangalia nani anamuita, alishangaa sana kumuona denis kijana ambae jana ya siku hiyo amepewa kipondo cha ukweli na Lucky, alijiuliza anataka nini kutoka kwake au ndo anataka kumpiga yeye ili amalize hasira za kupigwa na lacky.
" I'm Sorry Lucky, nadhani nimekushtua sana kukusimamisha bila kukuambia kama ntakuwa na mazungumzo yoyote na wewe. Alisema denis kumwambia maryam baada ya kufika karibu nae, jina lucky lilimshangaza bibie huyo kwani hakuwa yeye, kwa jinsi deniss alivyokuwa amechanganyikiwa hakufahamu kama anaeongea nae ni maryam hadi kumtamka Lucky.
" Mimi sio lucky deniss umechanganyikiwa?. Aliuliza maryam.
" Ooh God, okey i'm sorry maryam, Lucky yuko wapi?.
" Yuko room.
" Pliz nakuomba nionane nae naitaji kumuomba msamaha.
" Wewe weweee!, wewe deniss wewe!, kipigo ulichopewa jana hujaridhika unataka chengine ee!, ninachokuomba mpenzi wangu kaa mbali na yule mwanadada atakunyoosha, yule haombeki msamaha na kuna mambo yamemharibu kisaikologia ndo maana yuko vile, kaa nae mbali kabisaaa kwa usalama wako, ukimuona kimbia na usije kutaka kumfanyia mchezo mchafu wowote, jana beach huko kawakung'uta wanaume hao!. Alisema maryam kwa hisia akaonesha vidole vinne.
" Wanne. Deniss aliekuwa kimya kusikiliza kile anachopewa, alimalizia kwa kusema wanne.
" Enheeeee wanne babaangu kama wamesimama kawatembezea kichapo.
" Dah!, sikiliza maryam mimi siko kwa nia mbaya naitaji kumuomba msamaha yaishe tuwe kiamani, mambo ya uadui hayafai alafu sote tuko chuo inakuwa sii vizuri, naitaji kumuomba msamaha tafadhali mwambie. Alisema deniss huku tumbo likiwa joto kwa habari aliyopewa.
" Tatizo lako deniss uliitaji kujifanya bangi ukidhani amelegea, kumbe mwenzako bangi zaid yako sasa shauri yako, baada ya kupigwa ndo unataka amani, kama wewe ungempiga akaja kukuomba amani na ulivyokiburi ungemkubalia au ndo ungezidi kumtukana?.
" Usiseme hivyo maryam najua wewe ndo rafiki yake na ndo wa kunisaidia mimi pliz pliz nakuomba.
" mimi huo ugomvi bhana siuingilii, siuingilii kabisaa maana nguvu zangu zenyewe zinaitaji nguvu za ziada ili ziwepo, aya nimkoroge anigeukie mie anipe kipondo na mkono wake ulivyo haram kupiga vile unataka nife?, nashukuru tu kwa kuwa rafiki yake na kunikubalia urafiki. Kuhusu hilo jambo lako msubiri akiingia class umuombe. Alisema maryam. Muda huo huo lucky mwenyewe alikuwa anaingia eneo hilo, walikuwa karibu na kikorido na yeye alitokea kwenye kona hivyo walikuja kumuona akiwa tayari amewafikia, Deniss mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio akahisi kiyama kimemfikia alipomuona, kidume alitetemeshwa vibaya na mtoto wa kike ambae hakuonesha dalili zozote za kuwa mshari.
" Huyo hapo mwambie yale ulotaka kunituma. Alisema maryam.
" Mambo?. Alisema Lucky kumsalimia maryam.
" Poa ndo unaingia pindi?.
" Yah ndo naingia!, naona uko na hanisi la kiume.
" Mh!, lucky taratibu basi naomba upite uende class pliz my lovely friend.
" Nishikie mkoba wangu. Alisema lucky.
" Unataka ufanye nini?.
" Wee nishikie mkoba.
" Lucky usifanye hivyo bhana. Maryam alianza kulia lia akijua kabisa anataka ashikiwe mkoba ili alianzishe.
" Kama hutaki sema. Alisema kwa kufoce maryam ikabidi aushike, Deniss kukimbia alihisi ni aibu kubwa ikabidi abakie tu kibishi, miguu ilikuwa inatetemeka moyo wake ukawa hauna amani, hata kuongea nisamehe lucky alishindwa.
" Wewe ndo hodari wa kuwatukana watoto wa kike hapa chuoni sio?. Alisema lucky.. Mimi nawategemea mabwana wanikaze ndo nipate ada ya chuo room na kula si ndio?.
" Hapana. Alisema deniss kwa kutetemeka.
" Usiseme hapana kwa sauti ya kulegea hivyo wakati umeambiwa na dem ulietaka kumdhalilisha si kidume mwenzako, Nataka nikuoneshe huko kuwategemea kwangu mabwana kunavyonipa nguvu za kumshughulikia mtu, ntapambana na wewe kila ntapokuona kwa sababu tusi lako moyoni mwangu haliwezi kutoka, nlikukalia kimya mwaka mzima tokea naingia chuo ukiwa unanifata fata na kukuambia kiustarabu kuwa sitaki ukaniona fala, sikuwahi kukujibu vibaya kukutukana wala kukusonya, ila wewe ukajiona mdomo mrefu kwa ufahari wako ukaona umtukane lucky, tupigane ili ionekane kati yangu na wewe nani anawategemea mabwana hapa chuoni. Alisema lucky, kila alipokuwa akiongea munkari kichwani ulikuwa unapanda, alimkunja deniss nguo yake kifuani na kumuitaji wapigane ataeshindwa ndo atakuwa anategemea mabwana, maneno hayo yaliyozungumzwa na kijana huyo yalimuuma sana lucky kama mtu anaejielewa anapotukaniwa wazazi wake au mama yake, kwa hilo tusi la yeye kuwategemea mabwana chuoni alihisi ametukanwa tusi kubwa zaid ya mtu kumtukania mtu mama yake...
" Lucky naomba tusameheane, nakubali nlikosa ubinadam nisamehe yaishe. Alisema deniss kijasho kikiwa kinammiminika usoni hadi kwenye uti wa mgongo, sura ya lucky ilishachafuka uzuri wake wote uliisha.
" Kwa kuwa yamekufika shingoni ndo unaitaji msamaha, vipi siku uliyotaka kuniaibisha ningekuwa dhaifu si ungenichafua?. Usitake kumuonea mnyonge hali ya kuwa ukionewa wewe unaumia. Alisema lucky kwa sauti ya upole kisha akaanza kumshushia makofi ya adabu, yalikuwa yakuchanganya mwisho alimkamua kichwa bila kuhofia kuharibika kwa nywele zake alizokuwa ameziweka vizuri kwa mtindo wa kirihanna, Maryam machozi yalimtoka akaanza kulia akipiga piga miguu chini, kuamlia alikuwa hawezi ikabidi apige kelele ili watu wasogee, bahati nzuri au mbaya wakina tunu nao ndo walikuwa wanatokeza eneo hilo.
Walishangaa sana kumuona Lucky akiwa amemng'ang'ania mwanaume ambae walikuwa wanamjua vizuri kwa kujisifu kwake pamoja na kujidai kwa pesa alizonazo, Amina alishagawa penzi kwa kijana huyo tunu nae alikuwa kwenye harakati, hawakutaka kuamini hata kidogo kama ni lucky huyo huyo wanaemjua wao mkimya muda wote chumbani ndo anagawa dozi ya vurumai, watu walizidi kusogea taratibu mpaka maprofesa, walifanikiwa kuamulia huo ugomvi ila tayari deniss alikuwa ametoka manundu usoni, jicho la kushoto lilikamuliwa ngumi nzuri tu likawa limevimba kama ameng'atwa na nyuki, alikuwa hoi zaid ya siku ya kwanza.
" Ntakunyoosha mpaka ukihame hiki chuo mjinga wewe, ulilolitaka limekuwa na kama una hamu ya kutiwa vidole makalioni panakuwasha nambie ntafanya kazi hiyo na sii kunitukana, unayajua maisha yangu yalivyo?. Au ushoga ulionao huo wa kujipodoa wanaume wenzako wakutamani wakupige mizinga unadhani na wenzako wanao!?. Alimtusi matusi ya nguoni ya kumdhalilisha ambayo mengine ngumu kuyaeleza mbele ya pablic ya watu, wanafunzi waliokuwepo walishangaa sana uwezo wa lucky kuongea maneno mazito ya aibu wakati walimzoea kuwa mkimya, wengine walijisemea mioyoni mwao kweli muogope mtu mkimya akiamua anakuwa balaa kuliko muongeaji..
" Binti kwa nini unafanya upuuzi huu hujui kama ni utovu wa nidhamu na unaweza kuchukuliwa hatua za kisheria?. Aliuliza moja ya walimu wakubwa aliekuwa anaeshimika sana na wanafunzi, ndo alikuwa anaingia ofisini kabla ya kufika akakutakana na vurumai hilo.
" Haya ni maisha yangu binafsi, kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria itabidi wanaotaka kunichukulia hatua wajipange, kwa nini yeye isiwe kwa mwengine?. Kuna mtu yoyote nliwahi kumtukana au kumtolea maneno machafu why yeye, Profesa hamad nakueshim sana ila nadiriki kutamka mbele yako, Ama zake ama zangu, aondolewe yeye hapa chuoni au mimi, laa sivyo ntakula nae sahani moja kila ntapoonana nae hiyo ndo kazi, anayajua maisha yangu hadi anambie mimi nawategemea mabwana chuoni kusoma?. Nliwahi kumuomba hata shiling moja baada ya kupungukiwa, mbele ya pablic ya watu anaitaji kuniondolea heshima yangu nliyonayo chuoni nimfanyaje, mara ngapi nachukua tuzo za nidhamu ina maana gani, sina ina maana mwanafunzi mtiifu msafi na asiekuwa na tabia mbovu?, why anichokonoe?. I swea my professa mbele yako naapa popote ntapomuona Denis lazima nimtembezee kipigo, kwa kuwa nguvu ninazo uwezo ninao, atajua kuwa kuna wanawake vichaa walivuta bangi kabla ya kuzaliwa kwao sii wanaume tu.. alisema lucky kwa sauti ya kupanda na kushuka huku machozi yakimtoka kutokana na hasira alizokuwa nazo, hakujali maneno hayo anamuambia nani mbele ya umati wa watu ambao ulishakuwepo, Amina na tunu walikuwa katika mshangao mkubwa wa kujiuliza huyu ndo lucky ambae wanaishi nae chumbani kwao siku zote au sie ?

NINI KITAENDELEA KATIKA EPISODE YA 09 ? Kesho pita katika App yetu hii upate muendelezo wa uhondo huu.

Usisahau ku Share na marafiki wasome stori hii pia.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.