Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 7 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 7

Riwaya: SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA.
Mwandishi: SEID BIN SALIM
SEHEMU YA 07
Ilipoishia......
Hakuitaji kwendelea na mada hiyo, aliamini mtu mwenyewe anaeongea nae kichwa chake nusu zimo nusu hazimo, walienda hadi msasani wakapita moja ya duka kubwa la nguo kufanya shoping ndogo, walipomaliza walienda moja kwa moja beach kuangalia mazingira na kuogelea pia.
" Napenda sana kuogelea sijui na wewe vipi?. Alisema maryam wakiwa ufukweni mwa bahari.
" Sii saana. Napenda tu kuyaona maji na kuyachezea chezea basi.
" poa, mi nakuacha hapa basi naingia kwenye maji japo dakika tano nikatoe mikosi.
" Usijali kuhusu hilo best.
Alivua nguo zake akabaki na nguo za ndani, alitoa kimtandio kwenye mkoba akajifunga kiunoni chengine kichwani, lucky alimwangalia bibie alivyo na mwili mzuri wa kuvutia, alimsifia maryam akaelekea zake kwenye maji, alipofika alijitupa akazamia ndani na kwenda hadi kwenye maji makubwa.

Songa nayo......
Alikuwa anayajulia vizuri kuyachezea ya mbali na karibu, eneo alilokuwa analitumia kuogelea kulikuwa na kikundi cha vijana nao wakifanya yao, walipomuona mtoto mzuri anaoga waliitaji kumfata ili wakaoge nae, walimsogelea wakampa Hi, maryam hakupenda kitendo hicho akawaomba wakae mbali nae haitaji, walimng'ang'aniza wakawa wanamshika shika hasa kwa kuwa walimuona yeye peke yake hana mtu.
" Naomba mniache basi nyie vipi.
" Aaaah mtoto mzuri hutaki nini sasa?.
" Tueshimianeni kila mmoja anakuja huku kwa starehe zake tafadhali.
" Oya mnamuelewa huyu?.
Walimzunguka wakawa wanamtupia maji usoni huku wakiwa wanacheka kwa furaha, wengine walizamia chini na kumshika mapaja yake, maryam alilalamika haitaji kitendo hicho akawaonesha uso wa kuchukia lakini wapi, alipoona wamezidi ilibidi aanze kuwamiminia matusi ya nguoni bila kuogopa, vijana hao ambao walikuwa watano hawakufurahishwa na kitendo cha maryam kuwatukania wazazi wao na matusi mengine makubwa huku akijaribu kutoka kwenye maji, kila alivyojitahidi kutoka majini na wao walikuwa wanamfata wakimzonga na kumpatia vidonge vyake vya matusi makubwa makubwa, sauti zao zilikuwa zinapazika zinafika mbali, Lucky alisikia jinsi maryam anavyotukanwa na akaona alivyozongwa, alisimama na kujiuliza vipi akasogea karibu na maji yalipoishia, maryam nae alikuwa anakaribia maeneo hayo hayo tayari akiwa amefanikiwa kutoka majini.
" Hey guys vipi?. Aliuliza lucky.
" Vipi kivipi ndugu yako huyu?. Alisema kijeuri kijana mmoja.
" Nimeuliza vipi na wewe unantupia swali, mbona mnamzonga mwenzenu?. Aliuliza tena lucky.
" Huyu dem hana akili, tunamfata kwenda kuoga nae mtoto mzuri tupeane kampani anajifanya ni mzuri saaaaaana eti anakataa, tunamshika kidogo anatutukana tumemmaind sana haloo!. na wewe kama ni ndugu yake kaa mbali na sisi laa sivyo tunakushambulia na wewe sawa?. Alisema moja ya vijana hao lucky akaachia tabasam.
" Naombeni msimguse huyo mdada!, kama mna ubavu mnajiweza na nyie vidume kweli mnajiamini niguseni mimi. Alisema kwa kujiamini Lucky, maryam aliekuwa katika wakati mgumu alishangazwa na maneno ya lucky, vijana walionekana wameshiba wameshindikana lakini alisema nao kwa kujiamini.
" Mmemwelewa nyie huyu dem?. Alisema kijana mmoja aliejulikana kwa jina la Pita.
" Kwa iyo unaitaji uchezewe wewe au vipi. Alisema mwengine Seif.
Kutokana na walichoambiwa na lucky ikiwa vidume kweli wamguse yeye na sii maryam, walimsogelea na kuanza kumzunguka huku wakiamuangalia kwa dharau, seif alimshika kiuno chake pita akamshika shavu, hapo hapo lucky aliwachenjia na kuanza kuwacharaza makofi ya kushtukiza.

Waliona wameshindikana ila lucky alishindikana zaid, makofi yaliwaingia wakatumia wingi wao kuitaji kumshushia kipondo, bahati mbaya au nzuri hawakufanikiwa kwa hilo kutokana na utata aliokuwa nao Lucky, mwili ulikuwa ni wa kike tena umekaa kirembo, ila roho yake na misuli yake ilikuwa zaid ya mwanaume, kupigana na kiumbe kinachoitwa mwanaume hakuona tabu, pengine kuna wanaume aliwazidi nguvu za mikono.
Vijana walipoona mziki wa bibie hawauwezi, wakiendelea kuwepo watarudi makwao na alama, waliamua kutoa mbio wakiamini ndo kitu pekee cha kuwaokoa kwa kuwa haziuzwi, walichanganya miguu bila kuangalia nyuma, walifika sehemu wakachukua nguo zao na kuchanganya tena mbariga, walipofika mbele ndo walikaa sehemu wakaanza kusimliana kilichowatokea, kila mmoja alimweleza mwenzake maumivu anayojisikia.
" Haijawai kunitokea. Alisema seif.
" Kaka kuna wanawake wengine hawafai.
" Yani yale makofi aliyonicharaza nimehisi napigwa na izrael. Alisema Pita.
" Katika maisha yangu nlisema haitokuja kutokea nipigwe na dem ila leo nimekiona chamtema kuni.
" Na pale tusingechanganya mbariga alikuwa anatutoa alama..
Lucky na maryam nao walipoona vijana wameondoka walitoka beach huku lucky akimpatia pole maryam, kulikuwa hakuogeki tena furaha ya beach iliondoka, maryam alimwangalia lucky kwa jicho la tatu na kujiuliza ni msichana wa aina gani.

" Mh!, kweli wasichana tunatofautiana, wengine tunawaogopa wanaume wakitusogelea tu tumekimbia lakini wenzetu wanawateremshia kipondo duh. yani nkiwa na lucky hata saa tisa natembea bila woga, hakuna mambo ya kukerwa kerwa anapiga kama mwanaume!?. Alijisemea moyoni mwake, alienda mpaka sehemu za kuoga akaoga maji ya kawaida, alipomaliza alivaa nguo zake wakatoka beach, jua la jioni ndo lilikuwa linaishia, waliingia ndani ya gari wakainza safari ya kuelekea kwengine, kwa kuwa usiku ulishaanza kuingia maryam hakuitaji waelekee chuo kwanza, badala yake walienda mpaka maeneo ya sinza kulikokuwa na sehemu nzuri ya kupumzikia na dina nzuri, ili wapumzike kwenye mida ya saa mbili na nusu au saa tatu waanze safari ya kuelekea mlimani..
Alihakikisha anampeleka lucky sehemu ambazo zitamfanya kufurahi na kuinjoy, na kweli lucky alionekana kufurahi sana baada ya kuingia sehemu iliyokuwa finyu ya faragha, alikuwa hajawai kushuhudia kicheko chake lakini lucky kuna baadhi ya mambo aliyaona huku wakiongea na kumpelekea kucheka, waliinjoy sana maryam hakujuta kumtoa lucky out kwani hakumuangusha, maeneo hayo kulikuwa na burudani za muziki zinaendelea na wasanii wa mambo ya kuchekesha, vitu vilivyowafanya wachelewe kutoka, saa tatu waliyokuwa wameipanga hatimae ilikuwa saa tano, saa tano na nusu ndo walitoka na kuianza safari ya kuelekea chuo, kwa muda ulivyokuwa umeenda maryam hakuona umuhimu wa kurudisha gari nyumbani.

Saa sita kamili usiku waliingia katika geti la chuo wakakutana na magari kibao ya wanafunzi yakiwa yanatoka kwa sababu ya mambo ya weekend, walifika paking wakapaki gari lao wakafanya malipo ya ulinzi kisha kuitafuta njia ya kuelekea bwenini, ambayo waliifatisha ili iwafikishe room kulikokuwa na makazi yao.

" Nimefurahi sana leo, kiukweli sikutegemea kama itakuwa hivi, nakushukuru sana kwa kunifanya nijihisi mtu katika watu. Alisema lucky wakiwa wanatembea kidogo kidogo.
" mimi ndo nimefurahi zaid lucky.
" Kwa nini?.
" Ntakuambia kesho tukitoka class.
" Ok poa, Kesho una kipindi asubuhi sio?.
" Yah alafu tuko na profesa malki sasa.
" napenda sana masomo yake yule mzee.
"Ana elim ya saikology kichwani so anapofundisha lazima umpende tu, anacheza sana na vichwa vya watu.
" nakubali kwa hilo kwa sababu dah, huwa akiingia class kwetu moyoni hujihisi kupata furaha, nlivyochoka sasa yani nkifika ndani najimwagia maji nalala.
" Hatuna tofauti, nahisi mwili mzima hapa nlipo umezungukwa na kitu kizito.

Walipiga hatua moja baada ya nyingine wakiendelea na mazungumzo, waliingia kwenye majengo ya mabweni, waliambiana kiasi gani wamefurahi katika out yao, hasa lucky ambae alikuwa ana siku nyingi sana hajatoka, walipofika ndani waliingia kuoga kisha kupumzika, hawakuitaji kufanya lolote kwa muda huo, lucky alikuwa amechoka zaid ya sana, ilikuwa ni muda mrefu hajafanya mazoezi ya mwili, kila kiungo alihisi kinawaka moto, kitu kilichomfanya aitaji mapumziko ya muda mrefu ili kuwa sawa.

Hakuna kilichoendelea kwa usiku huo zaid ya usingizi, kipindi lucky anautafuta usingizi maryam yeye aliendelea kuwaza baadhi ya mambo aliyoyashuhudia kwa lucky.
" Kesho nkitoka class inabidi niende nyumbani kuongea na mama anambie kuhusu mzee edwad nimjue, uenda ndo mzazi wa Lucky.

Alijisemea moyoni mwake akavuta shuka kwa ajili ya kuanza kuutafuta usingizi, hadi kufika saa saba hakuna aliekuwa macho, Amina na tunu wao hawakuwepo, walikuwa wameenda sehemu za starehe kuisindikiza weekend, hawakuwa na mchezo na siku hiyo kwa kuwa nafasi yenyewe kuipata ni mara moja kwa wiki, siku nyingine zote wanakuwa bize na masomo.

NINI KITAENDELEA KATIKA EPISODE YA 08 ? Pita kwenye App yetu mara kwa mara kupata muendelezo wa simulizi hii tamu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.