Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 5 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 5

Riwaya: SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA.
Mwandishi: SEID BIN SALIM
SEHEMU YA 05
Ilipoishia......
" Mimi mjinga?. Alidakia deniss.
" Tena ni malaya usiokuwa na bi*** ya nyuma hanis wa kiume wewe, unanijua vizuri au unashoboka tu kwa sababu unamuona lucky kama lucky?. Aliuliza akiwa amekunja mikono, sura yake ilionesha kiasi gani amechafuka rohoni..
" Lucky naomba usiwe hivyo tuondoke utajaza watu hapa why hivyo!?.
" Maryam naomba usinipande kichwani na wewe, niache kama nlivyo naitaji kumuonesha huyu mjinga kati yangu na yeye nani anawategemea mabwana hapa chuoni, tena yeye hategemei mabwana, anategemea wanaume wenzake wamkaze ndo apate vijisent huoni anavyojipodoa?.
Songa nayo......
" Maryam unamuona rafiki yako asivyokuwa na adabu ee!!. Alisema deniss baada ya kusikiliza maneno ya lucky.
" Eh jamaniii why hiviii lucky pliz dia tuondoke potezea why!!.. Alilalamika maryam akigonga gonga miguu chini akasogea pembeni, miaka yote hakupenda ugomvi kuushuhudia machoni mwake.
" Yani umenivunjia cm yangu bado unantusi matusi ya nguoni namna hiyo. Alisema deniss.
" Hayo sio matusi, kama ni matusi basi umeyaanza wewe...? Alisema lucky akaongea vitu vyengine ambavyo havisemeki, vilivyopelekea denis kushindwa kustahamili na kumbamiza kofi la shavu la kushoto, Lucky ndo alizidi kuvurugika hakuitaji kushindwa, bila kujali kama yuko mbele za watu alimuingia deniss mwilini, denis alijaribu kujibu mapigo huku maryam akiwaomba watu waje kusaidia, lucky alikuwa kama mwanaume, katika hangaika alifanikiwa kumlaza deniss chini na kuanza kumpa ngumi za uso za shingo na masikio, zilikuwa ngumi ngumi kweli sii ngumi za kike kike, kilikuwa kipigo cha fedheha kwa deniss hata nguvu za kujitetea hakupata, alidhani lucky laini kama wanawake wengine au kuliko wanawake wengine wa chuo kutokana na ukimya wake wa muda wote, alichezea kipigo damu zikaanza kumtoka sehemu mbali mbali usoni, watu walisogea kuamlia ugomvi lakini hawakufanikiwa kirahisi kumwondoa mwilini mwa denis lucky, alimkandika ngumi za ukweli bila kumuonea huruma, sura ilikuwa inafuja kwa hasira macho yakiwa yamefinyika.
" Huu mbona ni upumbavu mnafanyiana nyie watu tatizo ni nini hasa?. Aliuliza bwana mmoja aliekuwa na mwili wa kibabe babe aliefanikiwa kumtuliza lucky, Denis alikuwa hoi analia kama mtoto, kidume kizima kilichokuwa kinajulikaana kwa kujinyodoa chuoni hapo kilipigika vya kupigika, ilikuwa ni aibu kubwa sana kwake, watoto wa kike walijaa eneo hilo, hakuna alieweza kuamini kama ni lucky aliefanya shughuli ya kukivujisha kidume damu, wengi walijiuliza imekuwaje kwani walimzoea kwa ukimya wake.
Maryam alieleza kila kitu kilivyokuwa, baada ya ghash ghash ndefu za hapa na pale, lucky aliomba asishikwe na mtu yoyote ugomvi ushaisha, alimsogelea deniss aliekuwa ameharibika usoni.
" Boy!, usione kila dem wa chuo mkimya kimya ukahisi amelegea na unaweza kumpelekesha unavyotaka, kaa mbali na maisha yangu na nimekwambia mara kadhaa nikome hutaki, kuyaondoa maisha yako na mimi nkatoeka kwenye dunia hii sii kitu cha kushangaza kwangu. Akili zangu ni mbili tu kichwani na nazijua mimi mwenyewe. Usiitaji nije nikupeleke kuzimu ukajuta kwa nini umezaliwa, Mamaangu tu duniani ndo nnamuheshim wengine wote vinyago, usitake kunirudisha nlikotoka wakati sitaki hata kupakumbuka, neno lolote ntalojisikia ntaongea kwa sababu hakuna nnae muogopa zaid ya Mungu, nshadata na maisha yangu na kama una uwezo nipeleke segerea mjinga wewe, umeitaji biff na mimi na nnakuapia Deniss Kokote ntapokuona iwe ndani ya chuo au nje ya chuo, Akkyamungu naapa ntakutembezea kichapo na hakuna wa kunigusa. Aliongea lucky machozi yakiwa yanamtoka kwa hasira alizokuwa nazo, kulishakuwepo umati mkubwa wa watu lakini hakujali, aliongea alichojisikia bila kuhofia, watu wenye heshima zao walifika na kumuitaji Lucky arudi chumbani kwake akatulie, mwisho alimuonesha deniss jeuri ya pesa kama yeye ndo anazoringia.
" Carefull with me deniss, i swea kama ndo hiki ulichokuwa unakitaka sasa umekipata, na kama unaringia pesa ulizonazo nakusikitikia sana, huna pesa una vijipesa, milioni moja na laki sita ni sawa na elfu moja tu kwangu, kama unashida nayo ntakupatia chek ya benk uende kutoa pesa unayotaka ukitosheka zitazobaki ziache. Usilete usupa star chuoni wakati wee ni wa kuja tu mshamba mshamba wa kijijini huko uluga ulugani..
Hakuna aliewahi kumuona lucky akiongea kiasi hicho, kilikuwa ni kindo cha kipekee huku wengi waliokuwa wanamdharau wakaweka heshima kwake, maryam nae hakutaka kuamini kama lucky anaweza kufanya vitu alivyovifanya, alijua labda ana tatizo la pesa kwao lakini ka milioni moja anaiona elfu moja ina maana ni sheedah!, walichukuana wawili hao wakatoka eneo hilo huku lucky akiwa gumzo kwa kila mmoja, Deniss maneno yalimuishia akapelekwa sehemu kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya sura yake, yote yaliyoongelewa na mtoto wa kike ni moja tu alilikumbuka kila wakati. UMEITAJI BIFF NA MIMI NA NNAKUAPIA DENISS KOKOTE NTAPOKUAONA IWE NDANI YA CHUO AU NJE YA CHUO, AKKYAMUNGU NAAPA NTAKUTEMBEZEA KICHAPO NA HAKUNA WA KUNIGUSA.
" kaka ilikuwaje hadi dem akakubalaguza hivyo ndugu?. Kijana aliekuwa anampatia huduma kwenye chumba cha matibabu alimuuliza.
" Acha tu ndugu yangu.
" Yani umeshindwa hata kujitetea mzee ukakubali kupigika.
" Yule dem atakuwa na mishipa ya kiume, kwa sababu zile ngumi alizokuwa ananipa nlikuwa nahisi napigwa na Anold au rambo. Alisema denis kijana akaachia kicheko. Usicheke Mwita, kama hayajukukuta huwezi kujifunza, nimejifunza kutoka kwake. Ujue ukiwa una elim tofauti na yule asiekuwa na elim. Ameahidi kuweka biff na mimi ila ntamfata nimuombe msamaha yaishe.
" Yaishe au unaogopa kutembezewa kipigo kila ukionekana?. Ila wee boya sana rafiki yangu. Dem kweli anakupiga. Hata meno basi ya kumtafuna umekosa?.
" Wee nipatie huduma bhna hayo mengine potezea, najua umekalia majungu tu. Alisema kisha akakaa kimya, kijana huyo aliejulikana kwa jina la mwita aliendelea kucheka kama mazuri, haikuwa kwake pekee, hata baadhi ya marafiki wa deniss waliishia kucheka kwa lililomkumba mwenzao, Lucky alikuwa midomoni mwa watu wote walioshuhudia tukio, kibaya zaid taarifa za ugomvi zilifika hadi kwenye ofisi za juu.
Lucky na maryam walirudi chumbani kwao wakawakuta amina na tunu nao wanamalizia kunywa chai yao, hawakuwa na taarifa yoyote kuhusu ugomvi uliotokea, waliwaangalia bila kuwasemesha maryam akaingia bafuni kwa ajili ya kujimwagia maji, Lucky alipanda kitandani kwake akachukua moja ya book lililokuwa la history akaanza kujisomea, hakusoma sana alichukua laptop iliyokuwa pembeni ili kuperuzi kidogo. kitendo cha kutoka kwenda hotel kunywea huko chai japo yalitokea maugomvi kilimchangamsha mwili wake, alijihisi nae mtu katika watu mbali na siku za nyuma alizozoea kunywea chai ndani tena bila kampani yoyote, kwa alivyoonekana ni kama mtu ambae hajapigana, na hasira zake zote ziliishia huko huko chini.
Maryam alimaliza kuoga akarudi akiwa na khanga nyepesi mwilini, baadhi ya viungo vyake nyeti vilitokelezea akakaa kitandani kwa kucky, aliangalia kile anachokifanya kwenye laptop ndani ya sekunde kadhaa, alimwangalia usoni moyoni akajiuliza kitu, alidhani uenda atamuona akiwa amevimba amenuna kwa alichokifanya chini lakini wapi.
" Naona uko kwenye bloggas. Aliuliza.
" Yes mamy.
Alipomsemesha na lucky kumjibu, Tunu na Amina walimwangalia kwa jicho zito kisha wakaangaliana, walinyodoa midomo yao wakaendelea kufanya yao.
" Nna wiki sasa hivi sijapitia huko modem yangu iliharibika.
" Ooh pole ilivunjika au?.
" Hapana, kuna siku nlikuwa nafua nkasahau kama ipo kwenye mfuko wa shart nlilovaa, nlipoinama tu ikaanguka kwenye maji, nliianika lakini kumbe ilishakufa.
" Ntakupatia moja utumie nnazo mbili.
" Ntashukuru sana, jiandae basi tutoke au umeghairi?.
Alisema maryam na kuzidi kuwashtua wakina tunu waliokuwa kimya wanasikiliza mazungumzo yao.
" Mbona mapema.?
" Yes nataka nipite home mara moja, nchukue gari twende shoping na mida ya beach itakuwa inafika.
" ok poa, kwa kuwa nimekupromose siwezi kukukatalia.
" kama ungekuwa hujanipromise?.
" ningekuruka futi mia siendi?.
" Ila wewe ujue ni mtu wa ajabu lucky.
" Kwa nini?.
" Kwa yaliyotokea chini huko sikudhani kabisa kama tutaongea hivi.
" Usijali kuhusu hilo.
" Hizo ngumi umejifunza au ni za kuzaliwa nazo?.
" potezea mambo hayo. Maryam aliitaji kujua baadhi ya vitu lakini lucky akamuitaji apotezee, kuna mambo aliyaona kwa binti huyo na kumvumbua sana akili, hasa msemo wake wa usitake kunirudisha nlikotoka, moja kwa moja maryam aliamini lucky kuna maisha flan alipitia yaliyomfanya asiwe sawa kiakili..
Waliendelea kuongea taratibu huku wakiangalia newz mbali mbali kwenye mablogz na website.
" Duh huyu kaka ana sura mbaya kama usiku. Alisema maryam baada ya kuiona picha mbovu ya mtu.
" Anafaa kuwa mmeo huyu!.
" Loh!, ntampitisha wapi mimi huyu muone mdomo wake.
Alisema kisha akaachia kicheko, lucky alitabasam, hiyo ndo ilikuwa cheka yake sana sana pindi anapofurahi. alitoka kitandani akamwachia maryam laptop akaingia bafuni kwa ajili ya kuoga, ilikuwa inakimbilia majira ya saa sita kasorobo, kitendo cha lucky kuingia bafuni kiliwafanya wakina amina wainuke vitandani kwao kuongea na Maryam.

NINI KITAENDELEA KATIKA EPISODE YA 06 ? Kesho pita katika app yetu hii itakuwa tayari imepostiwa.

SHARE NA MARAFIKI PIA.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.