Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 3 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 3

Riwaya: SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA.
Mw/Mtunzi: SEID BIN SALIM
SEHEMU YA 03
Ilipoishia......
" nimekuaribia usingizi wako ee, nsamehe mwaya!
" wala, nlishaamka zamani wala usijali kuhusu hilo.
" mapema yote hii.
" yah kuna masomo jana yalinichanganya ndo nlikuwa nayapitia, si unajua asubuhi kunakuwa hakujachanganya masomo yanaingia?.
" yah nalijua hilo, na wenzio vipi hao tayari au bado wameuchapa. Aliongea akiachia tabasam.
" wao bado wamelala.
" Ok poa, nakuomba ofisini kwangu mara moja basi nna maongezi na wewe samahani lakini. Alisema Sophia lucky akashangaa.
Songa nayo......
" ofisini kwako?
" Yah
" um, kuna tatizo lolote?
" Hapana lucky, ni mambo ya kawaida naitaji tuongee.
" ok sawa nakuja. Alijibu akiwa na wasi wasi wa kuhisi uenda jamaa zake washapeleka malalamiko, Sophia alimuaga na kumuitaji asichelewe kisha akaondoka, lucky alirudishia mlango akasimama katikati mwa mlango na kuangalia vitanda walivyokuwa wamelala wenzake, alitembea taratibu mpaka bafuni ambako alitoa khanga yake na kubaki mtupu, aliachia maji akavuta sabuni, alitengeneza nywele zake zisije kuingia maji, alianza kujimwagia kidogo kidogo huku akilini akijiuliza maswali mengi ambayo hakuwa na majibu yake.
Alimaliza kuoga baada ya kutumia dakika tano hadi sita akiwa bafuni, alivaa nguo haraka haraka akatoka kuelekea ofisini kwa Sophia, akiwa njiani cm yake ilianza kuita, kuangalia kwenye screen alikutana na jina la baba yake, badala ya kupokea na kuwa na furaha kama wanafunzi wengi wa hostel wanapokuwa wanapata bahati ya kupokea cm toka nyumbani, aliikata na kuzima moja kwa moja sura yake nayo ikibadilika kutoka katika mwonekano wa kawaida hadi mwonekano wa chuki.
Alifika kwenye chumba cha Sophia akapita hadi ndani, Sophia aliacha kazi zake alizokuwa anazifanya ili aweze kuongea nae.
" karibu sana lucky.
" asante nshakaribia
" nimemaliza kupata kifungua kinywa umechelewa.
" wala usijali kuhusu hilo.
" Uhm mpenzi!, nimeletewa malalamiko hapa na wenzako, kuwa unavyoishi ni tofauti na wao kabisa kwa nini?. Aliuliza Sophia.
" nlijua tu unaniitia hilo mumy, kiufupi hayo ndo maisha yangu nliyoyachagua kuishi sophia, kila mmoja ana style yake inayomfaa katika maisha, maisha ya chuo nayajua nkianza kujichanganya sitosoma wakati naitaji kufika mbali. ili mradi simtukani mtu, sigombani na mtu, simjibu vibaya mtu, wana haki ya kuishi kivyao na mimi kivyangu, nkiamka nawasalimia, tukinunua chakula tunakula wote wakikosa pesa wakanambia nawapatia. furaha yangu ni kitabu madam mengine siyaitaji. Alisema lucky na kumuacha Sophia njia panda, hakujua ashike wapi aache wapi kwani maelezo yake yalikuwa majibu mazuri tosha, hakuwa na la kuongezea alimwambia amerizika na majibu yake, waliongea mambo mengine huku lucky akimsisitizia kwa kumwambia kuna watu wanapenda kujua binadam wenzao wanaishije ili wawapande kichwani lakini kwake hilo haliwezekani.
Sophia alimruhusu arudi chumbani kwake, dada huyo ni mwanamke aliekuwa na akili nyingi sana za kumtega mtu, kilichokuwa kichwani mwake baada ya kumruusu aondoke alikijua yeye, ila muda waliotumia kuongea na maongezi waliyoyazungumza na jinsi walivyokuwa wanaongea, alipata kufahamu kuna tatizo linamsumbua bidada lucky japo haitaji kulionesha.
" Unaonekana mpole na mtaratibu lucky ila una tatizo linakusumbua na mimi ntalifanyia kazi mpaka nlifahamu.. alisema peke yake.
Lucky alirudi chumbani akawakuta wenzake bado wamelala, aliwaamsha akawakalisha kitako kutaka kujua kitu gani kimewakuta hadi kwenda kwa Sophia kumweleza matatizo yake.
" Friends, nawaeshim na mimi naomba mnieshim, msione kwa kuwa nakaa kimya siongei mkajua ni mjinga na zoba kiiivo tafadhalini, kila mmoja ana maisha yake ya kuishi, na kila mtu hapa amekuja kwa pesa zake na akili zake, hivyo sitaki mniingilie kwenye maisha yangu, nkiwatukana nendeni mkaseme, lakini ili hali siwatukani siwadharau tafadhali tueshimiane, kama hamuitaji kuishi na mimi semeni na kama mnahisi nawanyima uhuru waambieni wawapatie chumba kingine mniache peke yangu kwa sababu uwezo wa kulipa chumba kizima hiki nnao, msitake kunipanda kichwani nawaombeni na nawaombeni tena, maisha yangu hamyajui niacheni kama nlivyo. Alisema kwa hasira.
" lakini lucky!, kitu gani sisi hapo tumekosea?. Tunaumia tunapoona unaishi kiunyonge mpenzi, usituchukulie vibaya unajiathiri kisaikolojia lucky. Alisema maryam.
" siitaji niacheni niaribike kisaikolojia, naishi nitakavyo na sii mtakavyo Hey!, kwani lazima?. Alisema lucky.
" Basi dada yaishe, tusamehe kwa kirehe rehe chetu cha kutoa kwaito zetu hapa hadi kwa Sophia. Alisema tunu.
" ila na sisi umbea umetuzidi una haki ya kutuchamba. Alidakia Amina.
Tunu na amina walisimama wakavaa nguo zao na kutoka nje wakiwa wamepandwa na hasira kwenda kumwangalia mhudumu ambae huwa anawapatia chai, walimtaka maryam avae waende ila akagoma, walitoka chumbani akabaki maryam na lucky, maryam alikuwa ana huruma sana alijisikia vibaya namna mwenzake alivyo lalamika, hakutaka amuaminishe kuwa yeye ni mbaya wake.
" lucky, sijafunzwa kumuacha mtu anaelia akiendelea kumwaga machozi yake na mimi kutoka nje, maneno yako yanaonesha kiasi gani umekasirika juu ya maamuzi yetu, tokea uingie humu sijawai kukuona ukiongea hivyo, naomba unisamehe sana kwa kufanya kitu ambacho hujaridhia, nisamehe mimi na wenzangu, siko happy kiukweli kukuona ukiuzunika japo itanilazimu sasa. alisema maryam.
" Hivi unajua huyu dem simwelewi Amina ee!. Baada ya kuwa wako nje Tunu alisema kumwambia mwenzake.
" hata mimi, eti nna uwezo wa kuchukua room nzima peke yangu msiniingilie, Haa!, huyu wakuja nini.
" linavyoongea sasa kama mdomo umemeza flash, yani hata yale mapozi hana.
" kaniharibia siku asubuhi asubuhi Akyamungu, sijui mudi kama ntamkuta aniletee bia nipoze akili kwanza. Alisema amina akipeleka mkono kichwani kukuna nywele zake zilizokuwa tim tim flan.
" tena sio moja, huyu mtoto mimi nataka nimchangamkie nimkorogee Kiswahili ajione kama kunya, eti hooo mna maisha yenu na mimi nna maisha yangu yani kaniboaaa. Alisema tunu.
" ila kirehe rehe chetu na sisi, ashuo gani hadi midomo ikatupwaya kwenda kusema?.
" kirehe rehe kihere here mwenzangu na nimekoma kuingilia maisha ya watu yasiyonihusu. Alisema tunu. walifika chini walikokuwa wanapatikana wahudumu wakamuona mudi waliemzoea, walimpatia maagizo ya nini awapalekee kisha wakageuza kurudi.
Maryam ndani aliendelea kumuomba msamaha lucky ili amsamehe kwa kumfanya akose raha baada ya kuchukuana na wenzake na kwenda kwa sofia, lucky alimwelewa akamwambia asijali ni mambo ya kawaida.
" Ok my friend, napenda kuiona furaha ya mtu, sipendi kuipoteza maana najua siwezi kuilipa. Nambie ungependa kula nini morning hii!. Alisema maryam mara alipoona tabasam la lucky, aliinuka kitandani akaweka mkono kwenye mfuko wa nguo yake iliyokuwa umetundikwa kwenye henga kuangalia kama kuna pesa.
" Sijisikii hata kula kitu mumy usijali.
" No Lucky, asubuhi lazima kuwepo na kifungua kinywa, kama umenisamehe naomba unambie utakula nini!. Alisema akiachia tabasam, mkononi tayari alishikilia shiling elfu 10 ya kitanzania.
" Unataka kwenda kuagiza?. Aliuliza lucky
" Yes.
" Poa, nchukulie soseji mbili, chai ya maziwa juis na chapati moja.
" Ok poa.
Alitoka maryam kwenda kuchukua chai, alipofungua mlango akakutana na wakina Amina wao wakirudi.
" ulikuwa bado unaongea na huyo mtu?. Tunu alimuuliza.
" yah nlikuwa naongea nae.
" ana jipya gani.
" katusamehe.
" kwani tumemkosea.
" Tunu acha hizo bhana, huoni kama tumemkosea kwenda kwa sofia bila kumwambia?.
" Duh!. Tunu alitoa macho ya mshangao.
" Ujue tunu huyu nae ndo wale wale huruma huruma. Alidakia Amina.
" sio huruma huruma, ili hali hatutukani, tukimsalimia anajibu vizuri, kwa nini tumuingilie katika maisha yake?. Tumuache kama alivyo. Alisema maryam.
walipomuangalia maneno yake wakajua tayari yupo kwa ajili ya kumtetea lucky, walimruhusu aendelee na safari yake ya aendako nao wakaendelea kuwepo nje kupiga umbea kabla ya kuingia ndani.
" Kashakuwa rafiki yake huyu. Alisema amina.
" Muache akizingua na yeye si tunamsheet tu.
" Anajifanya huruma huruma, wee lini paka na mbwa wakakaa pamoja bila kukoromeana?. Jitu liko kama zombie halijua kuongea, muda wote kuvimbisha mashavu tu kama kabugia pili pili urafiki nae wa nini?.
" ndo hapo sasa!, hata mi nashangaa.
Walimaliza kuongea wakaingia ndani na kumkuta lucky yuko kitandani amelala, tayari alikuwa kwenye mkusanyiko wa mawazo, machozi yalikuwa yanamtiririka upande upande, walimuangalia hawakuitaji kumshtua, kila mmoja alipanda kitandani kwake akachukua cm na kuanza kuchart, waliweka phoni maskioni wakawa hawana habari wasijue kinachoendelea, lucky alikuwa katika wakati mgumu sana, hakuacha kukumbuka baadhi ya mambo yaliyomtokea nyumba ambayo yalisababisha mara kadhaa kumfanya akose raha na kuachia kilio cha bila kutaka wala kutaraji.
Maryam alirudi baada ya kuagiza vya kuagiza, akiwa mlangoni aliwaangalia amina na tunu akaona ambavyo hawana habari na mtu wako bize na kusikiliza miziki, alipomuangalia lucky akajua tayari hayuko sawa, alitikisa kichwa chake kumsikitikia, ni yeye pekee alibakia kumuonea huruma, alisogea akakaa pembeni ya alikolala.
" Lucky. Alimuita kwa sauti ya taratibu, lucky alishtuka akafuta machozi yaliyokuwa yanatoka.
" Usijaribu kufuta chozi la kinyonge wakati haiwezekani. Mbona unajaribu kuficha maradhi ya kidonda cha nje ya mwili wakati kila mmoja anakiona?. Sii vizuri lucky unavyofanya, hali yako hainiusu lakini naumia kuona wenzio tunafurahi wewe huna furaha. Alisema maryam katika hali ya huzuni baada ya kuona lucky anafuta machozi, lucky maneno aliyoambiwa na binti huyo yalimuingia akilini, aliinuka akakaa na kumshika pajani.

NINI KITAENDELEA KATIKA EPISODE YA NNE ? Kesho pita katika eneo hili hili itakuwa tayari imepostiwa muendelezo. Usijaribu kupitwa. Pakua App Yetu Uisome Kiurahisi Zaidi. >>BOFYA HAPA<<

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.