Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 2 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 2

Riwaya: SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA.
Mtunzi: SEID BIN SALIM
SEHEMU YA PILI
Ilipoishia...
" hhhhhmmmmm. Aliguna tunu, kumbe na wewe umo?. Walinyanyuka na kicheko kila mmoja akabeba mkoba wake na kwenda darasani. lacky alitoka bafuni akiwa na khanga moja mwilini akakaa kitandani na kujifuta futa maji, hakukaa dakika akanyanyuka na kusogea kwenye kioo kujiangalia mwili wake wote ulivyo. Alivuta mafuta aina ya lotion akajipaka baadhi ya sehemu za mwili wake, alipomaliza aliitoa khanga mwili ukabaki utupu kisha akavaa nguo za ndani zilizokuwa kwenye henga..
Alimaliza kwa nguo za chuo akabeba mkoba na kutoka ndani, hadi anafika darasan hakuna alieweza kumpa hi kwa sababu ya kusikojulikana sana na watu, kwa alivyokuwa anajiweka hakuna aliweza kumzoea kwani hata mbinu ya kumuingia haikuwepo, wapo wanaume waliojifanya midomo mirefu kutaka kuingiza mistari ya kumtongoza kutokana na uzuri wa mvuto aliokuwa nao kuanzia sura hadi maumbile, lakini walijikuta wanashindwa na kujionea aibu namna ambavyo lucky hakutaka upumbavu..

Songa nayo......
Masomo yalipoisha wanafunzi waliokuwa wanamaliza vipindi walitoka madarasani akiwemo mwenyewe lucky, mkoba wake ulikuwa begani bila kuongea na yoyote akashika njia ya kwenda kwenye chumba anachokaa, alisimama ghafla baada ya kusikia sauti ya kiume inamuita, aligeuka akakutana na sura ya moja ya wanaume ambao huwa wanamsumbua sana chuoni hapo kumuitaji kimapenzi.
" Samahani lucky kwa kukusimamisha.
" Bila samahani.
" Leo tumebahatika kutoka mapema darasani, vipi tunaweza kuwa pamoja lunch mchana?
" Hapana haiwezekani.
" Kwa nini lucky.
" Sina sababu ila haiwezekani.
" Hivi unajua kuwa wewe ni msichana mrembo ambae kila mwanaume hapa chuoni anakumezea mate?, ila sijawai kukuona ukiwa na mchanganyiko wa mtu yoyote Yule kuanzia wanawake wenzio mpaka wanaume kwa nini?
" Hiyo ni moja ya sehemu za maisha yangu, ndo style nlopanga kuishi, alafu usiishi kwa kukariri kuwa kila mwanamke alopewa uzuri lazima awe na mchanganyiko wa watu, uzuri wangu haumaanishi kuwa kila mmoja anaeniita niitike.
" Ok lucky, mi nkutakie siku njema ila ningeomba kupata japo namba yako ya cm, nadhani ntajiona mwenye bahati sana.
" Samahani Denis pia haiwezekani kupata no yangu.
" dah, ok poa good day
Lucky aligeuka na kuondoka zake huku nyuma akimuachia lawama nzito kijana aliejulikana kwa jina la denis namna alivyokuwa anatingisha mauno yake aliyojaaliwa na Mwenye Ezi Mungu, kijana huyo hakuweza kugeuka kirahisi hadi alipoona lucky ameishilizia ndo alianza kutembea, moyoni alikuwa na umivu kali la kukosa bahati ya kupata walau namba ya lucky msichana alievutiwa nae tokea anajiunga nae siku ya kwanza darasani.
Bibie alifika chumbani kwake akaweka begi kwenye kiti akajitupa kitandani, alilala chali macho yakawa juu na kuingia katika wingu zito la mawazo, dakika kumi mbele tayari alikuwa anabubujikwa na machozi ambayo hakufahamu yanatokea wapi, marafiki zake anao kaa nao waliingia kipindi hicho hicho bila yeye kusikia hata mlango ukifunguliwa, uenda kutokana na kuwa mbali kimawazo, tunu maryam na amina walisimama vizuri mlangoni kumwangalia kwa makini, walipoteza zaidi ya dakika nzima wakashuhudia jinsi anavyobubujikwa na machozi, huruma iliwaingia wakamsikitikia kisha kumsogelea taratibu, maryam alifika karibu nae akakaa pembeni yake na kumshika pajani, lucky alishtuka akawaangalia na kuanza kufuta machozi.
" why lucky why my dia, alisema maryam kwa uchungu, kwa nini unatufanya kama watoto lakini, kitu gani kinakusumbua moyoni mwako hadi sasa si utuambie jamani mbona unakuwa hivyo?. Aliuliza maryam.
" Hamna kitu maryam. Lucky aliongea shot akamuweka katika kipindi kigumu cha kumkatili moyo maryam.
" dah, mi ni rafiki yako lucky, nakuomba usinifanyie hivyo nakupenda, naumia sana nnapokuona katika hali hii, sema kama unaumwa tukupeleke hospitali mbona marafiki zako tunakupenda sana why wewe huoneshi upendo kwetu?. Aliongea kwa uchungu maryam lakini lucky hakuwa tayari kuongea chochote, maryam nae alianza kulia baada ya kuona ni kama vituko wanafanyiwa na binti huyo wanae ishi nae chumba kimoja bila ishara ya kuonesha kabisa kuwa nao, tunu aliingilia kati akamzuia maryam kulia, walichukuana wote watatu wakatoka nje, walisimama na kuanza kushauriana nini wafanye juu ya rafiki yao japo walishaamua kumtoa thamani ikiwa yeye haoneshi ushirikiano nao, ila hali waliyomkuta nayo ilibidi wabadili mawazo yao na kutafuta mbinu ya kumsaidia kumwondoa katika janga alilonalo.
" kiukweli hali ya lucky mi inanichanganya sana siwachifi, yani bora kuishi na nyoka ikawa inakudonyoa tu uenda maumivu yataisha kuliko kuishi na mtu wa aina hii Akyamungu. Alisema maryam.
" maryam unajiumiza kichwa tu my dia, hadi machozi yanakutoka kabisa kwa mtu kama huyo. Alisema amina.
" sijafundishwa hivyo mamy, roho yangu ni nyepesi sana nnapomuona mtu anateseka kwa kitu kisichojulikana.
" mimi nna wasi wasi lucky ametokea kwenye maisha ya shida sana, au hapa mjini ni mgeni maana kila kitu hajiwezi, story hawezi, kampani hakuna, kicheko kwake hakijawai kuonekana, kuongea na mwanaume hapana, sa si tumchukuliaje, ujue anazingua sana huyu dem. Alisema tunu.
" Anazingua anazingua!!!, ila nna wazo. Alisema Amina.
" wazo gani. Aliuliza maryam.
" twende tukapeleke malalamiko kwa msimamizi kiranja.
" Good, aidia nzuri sana hiyo, twende huko huko tumueleze kuwa mwenzetu hatumuelewi tumpe A to Z. alisema tunu.

Wazo hilo lilipita kwa wote wakatoka taratibu hadi sehemu alipokuwa msimamizi wa wanafunzi wote chuoni hapo, alikuwa mwanadada aitwae Sophia wakakaa chini na kuanza kumpa moja mbili tatu kuhusu lucky, lucky mwenyewe hakuwa anajua chochote wanachofanya watu anaoishi nao chumbani, alijipozea tu kitandani wimbi la mawazo likizid kumtafuna..

" Dada Sophia tumeishi na mwenzetu lucky mwaka sasa, lakini kwake hatujawai kuona kicheko, tabasam, furaha zaid ya huzuni, kilio kisichoisha, na ukimya basi, tunahisi atakuwa ana kitu kikubwa sana akilini mwake kinachompelekea kuwa hivyo, ila sasa hali yake inatutesa, kama kuna uwezekano mhamisheni hata chumba au kaa nae chini umsomeshe umpike akueleze kinachomsumbua au abadilike si hatuwezi kuwa na mtu wa aina ile, wee mtu kicheko tu kwake ni kama sikukuu, aka! sisi hatuwezi dada Sophia, pia tunamuonea huruma maana si usiku si mchana yeye na kilio ndo nini sasa?. Alisema amina akitumia zaid ya dakika kumi kuongea, kila kitu kilichokuwa kinaendelea kwa dada lucky alikiropoka mbele ya Sophia ili kuangalia kama uwezekano wa kutatua tatizo lake utakuwepo au laa.

" Mmekaa nae mwaka sasa katika hali hiyo kwa nini hamkufanya hivyo kipindi cha nyuma mfanye sasa?. Aliuliza Sophia baada ya kumsikiliza amina kwa makini.
" sa sisi tulikuwa tukimuangalia tu labda atabadilika lakini wapi. Alisema Amina.
" mmejaribu kumkalisha chini kumweleza?.
" ndio tena sii mara moja wala mara mbili.
" ok sawa nimewasikia ntalifanyia kazi.
" tena ukikaa nae mwambie kabisa tumechoka, wee jitu halijui hata kucheka bhna. Alidakia maryam akaongea kwa hasira.
" sawa nimewaelewa rudini chumbani kwenu. alisema Sophia kwa muonekano wa kuwa mkali kidogo, ila hawakushtuka ilikuwa kawaida yake, waliinuka kurudi chumbani kwao kabla ya kufika kokote tunu aligeuka.
" bora umwite sasa hivi uongee nae maana yuko analia huko chumbani.
" naomba mrudi kwenye room yenu tafadhali.
Hawakumuongelesha lengine walitoka wakatembea hatua kadhaa ambazo ziliwafikisha room, lucky tayari alikuwa ashamaliza kulia muda huo alikuwa amekaa kitandani anajisomea, pia hawakushangaa kwani ilikuwa moja ya kawaida zake, walipita kila mmoja akapanda kitandani kwake wakatoa cm zao na laptopz kwa ajili ya kuanza kuchart na kuperuzi katika mitandao mbali mbali.
Lucky aliwaangalia akatingisha kichwa na kwendelea kujisomea huku wao wakiwa wanachart, masaa yalisonga mbele siku ikaisha na kuingia siku nyingine, ilikuwa jumaa mosi kulikuwa hakuna anaeingia darasani, kila mmoja alichelewa kuamka isipokuwa lucky alieamka saa moja na kuingia katika dimbwi zito la mawazo, mlango uligongwa akashtuka na kujiuliza nani anawagongea mlango asubuhi yote hiyo wakati dada wa usafi huwa anaingia saa mbili na nusu. Uligongwa tena akaweka khanga yake vizuri aliyokuwa ameiegesha tu mwilini kisha kuinuka kitandani, alisogea hadi mlangoni akafungua na kuchungulia nani anagonga, macho yake yaligongana na macho ya Sophia kiongozi wa chuoni hapo, woga ulimuingia mapigo ya moyo yakaamka akamkaribisha huku moyoni akijiuliza mbona Sophia yuko hapo kwa muda huo.
" asante nshakaribia mambo? Alisema Sophia baada ya kukaribishwa.
" poa
" nimekuaribia usingizi wako ee, nsamehe mwaya!
" wala, nlishaamka zamani wala usijali kuhusu hilo.
" mapema yote hii.
" yah kuna masomo jana yalinichanganya ndo nlikuwa nayapitia, si unajua asubuhi kunakuwa hakujachanganya masomo yanaingia?.
" yah nalijua hilo, na wenzio vipi hao tayari au bado wameuchapa. Aliongea akiachia tabasam.
" wao bado wamelala.
" Ok poa, nakuomba ofisini kwangu mara moja basi nna maongezi na wewe samahani lakini. Alisema Sophia lucky akashangaa.

NINI KITAENDELEA KATIKA EPSODE YA TATU ? Kesho pita katika eneo hili hili itakuwa tayari imepostiwa tayari.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.