Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 1 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 1

SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA

Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA KWANZA
Mwaka mmoja ukiwa umepita tokea binti mwenye umri wa miaka 24 lucky ajiunge na chuo kikuu cha dar es salam UNIVERSITY OF DAR ES SALAM. Marafiki zake aliokuwa anakaa nao chumba kimoja katika hostel waliojulikana kwa majina ya Mariam, Tunu, na amina. Asubuhi na mapema ya wiki end waliamua kumkalisha chini rafiki yao huyo kwa ajili ya kuongea nae mambo flan, kutokana na jinsi walivyokuwa wanaishi nae katika hali ya unyonge na kuonekana hapend kushirikiana na mtu yoyote kimasomo hd starehe za hapa na pale.

waliishi nae kama sio mwenzao, walipoitaji ushirikiano wake hakuitaji kuwa nao, muda mwingine walimshuhudia akikaa kiupweke hadi kutoa machozi kwa muonekano wa kuwaza mambo mazito aliyonayo moyoni mwake, walimuonea huruma hasa kwa sababu wao ni watu waongeaji, walimkalia vikao vya kimya kimya walipopata nafasi ya kipeke yao, lakini namna siku zilivyozidi kwenda ndivyo lucky alizidi kutia huruma na kuishi katika mazingira ya kuusononesha uso wake, uvumilivu uliwashinda na kuamua kumkalisha chini ikiwezekana awaambie chochote kinachomsumbua moyoni mwake uenda wakawa na ushauri wa kumshauri.

" Lucky mpenzi, kikao hichi ni kwa ajili yako, tumeacha shughuli zetu ili tuongee nawe, tumeishi hapa mwaka sasa, lakini mwendo wako na wetu ni vitu viwili tofauti, kuna muda tumekushuhudia ukimwaga machozi bila sababu, mawazo yasiyoisha, huzuni wasi wasi na vingine kama hivyo, kitu ambacho kimetushinda kiukweli, kwa sababu sisi wakati wote ni watu wa kufurahi, kucheka, kununa kukasirika hatujui. so tunaumia sana tunapoona mwenzetu tunaeishi nae chumba kimoja hauko kama sisi, huoneshi furaha hata siku moja, tunaomba utueleze kitu gani hasa kinasumbua maishani mwako tafadhali.. Tunu aliekuwa pembeni yake alimuuliza akiwa amemuangalia kwa kushika mkono kwenye tama, lucky mwenyewe alishikilia mto uliokuwa mapajani mwake, machoni akionesha hayuko nao, mariam na Amina walikuwa wamekaa katika kitanda cha pili wakimtizama kwa macho yasiyoisha huruma.

" tunaomba utuambie kitu gani kinakusumbua maishani mwako, sisi ni marafiki wema, au tokea uingie hapa kuna jambo lolote baya tumekufanyia linalokufanya uwe hivyo?. Aliuliza Tunu lucky akatingisha kichwa kuashiria hamna. sasa kwa nini unatufanyia hivyo hatupendi lucky, twambie nini kinakusumbua hatuitaji uwe katika hali hiyo.

" Hapana Tunu mimi sina tatizo lolote. Alisema baada ya kupitisha mkono machoni kutoa machozi yaliyokuwa tayari yanamlenga.
" Lucky unajaribu kuficha ugonjwa usiofichika, hapo tu tayari machozi yanakutoka kisha unasema huna tatizo, tuko wanne tu hapa, zaid yetu hakuna mwengine anaetuona wala kutusikia tuambie tafadhali.. alisema dada mwingine Mariam ambae walipendelea sana kumuita Baby Mimah.
" mtoto koma mwengine yupo anaetusikia. Amina Alidakia maneno ya mimah.
" Ushaanza nani anatuona hapa?. Aliuliza mimah kwa kushtuka, amina kidogo alikuwa shambenga asietaka kitu kimpite.
" Sir God, anaona hadi uvunguni kama hujui.
" nlijua tu utasema hivyo, usilete matani wakati tuko serious bhna, unaichukulia baridi hali ya mwenzetu eee?
" Hapana kazi na dawa, kucheka kidogo kununa kidogo maisha yanaenda, bby lucky tunaomba utuambie basi kitu gani kinakusumbua mamy, ujue kukaa na tatizo moyono si kutatua tatizo ee. Alisema Amina.
" Sina tatizo mimi Amina niko kawaida.
" tatizo unalo, ujue hapa chuoni kuna kamchezo kabaya kanaendelea japo kwa upande mwengine kazuri, tukikuona hivyo hatukuelewi tutaenda kushtaki kwa calacte., so bora utuambie sisi mpenzi umbea utabaki humu humu ndani. Alisema amina huku akiwa amewaangalia wenzake.
" nawaomba hali yangu msimwambie mtu yoyote, siitaji watu wajue nnavyoishi, haya ndo maisha yangu tokea niko nyumbani. Alisema lucky akiwa ameangalia chini, waliendelea kumshawishi ili awaambie kile walichokuwa wanakiisi tokea kwake lakini wapi, mwisho waliamua kuachana nae wakimsihi sana abadilike laa sivyo watashindwa kuishi nae, upweke anaoweka hawauwezi kutokana na jinsi walivyozoea kucheka na kila mmoja..
Siku zilisonga mbele maisha ya lucky yakiwa hayo hayo ya ukimya muonekano wa msongamano wa mawazo na kujipwekesha na wenzake, ilifika sehemu wenzie anaolala nao walichoka ikabidi wamfate tena kumuweka chini lakini hakuna kilichobadilika, jinsi alivyokuwa anakaa alifanana na msaka tonge anaesaka tonge lake katika wakati mgumu wakati anatoka moja ya familia za kitajiri mno jijini DAR ES SALAM..
alivyoishi chuoni hapo lucky ( UNIVERSITY OF DAR ES SALAM ) walimu wengi walitokea kumpenda na kumjumlisha ndani ya daftari la wanafunzi bora mfano wa kuigwa na kila mmoja, kipindi chote cha mwaka mzima alibahatika kupokea tuzo ya mwanafunzi msafi na mwenye nidhamu kuliko wote, hakuna alichoambiwa na walimu afanye akakataa labda kiwe kibaya, alikuwa mtiifu kuliko watiifu, upole huruma kwa wanafunzi wenziwe pamoja na muonekano wa kudel na masomo wakati wote hata alipokuwa chumbani.

Wengi walipendelea mambo ya michezo wanapokuwa hawana ratiba yoyote ya masomo, au kutumia muda huo kwenda kula bata sehemu mbali mbali maclub na kwengine, lakini yeye vitabu vilimkoma baadhi ya wanafunzi wakawa wanamuonea wivu, tabasam kwake ndo kilikuwa kicheko tofauti na wengine, hakuna alichokiitaji zaidi ya kusoma, pale alipochoka alipanda kitandani kulala, lakini moja ya kawaida yake ambayo anaolala nao waliizoea, hawez kulala mpaka machozi ya mawazo yamtoke, kitu kilichopelekea waamini uenda alipitia kipindi kigumu cha maisha ndo maana analia kila wakati.
Hakuna alieweza kujua kama lucky anatoka kwenye familia ya kitajiri sana uenda kuliko wanafunzi wote chuoni hapo, hakuwa akijionesha kuwa kwao uwezo upo tena mkubwa, alionekana mwanafunzi wa kawaida kuanzia mavazi, misuko ya nywele na vitu alivyokuwa anatumia.

Familia yake yote ilikuwa ikiishi pembezoni mwa jiji la dar masaki karibu kabisa na bahari ya hindi, mama yake aliejulikana kwa jina la jenipha alikuwa mganga mkuu katika hospitali ya mhimbili, kaka yake anaemfata alikuwa mmiliki wa makampuni matatu ya usafirishaji madini kwenda nje, huku baba yake mzee edwad akiwa mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa..

Utajiri wa familia hii ulikuwa mkubwa mno kuliko hata wa viongozi waliokuwa madarakani. Iliishi kwa upendo muda wote, majirani waliiangalia kwa jicho la tatu namna inavyoishi, waliyatamani maisha yao wanayooneshana wakiwa nje, kitu kilichokuwa tofauti kwa mama mwenye nyumba jenipha aliekuwa anaiona bora jana kuliko leo, ila haikuonekana hivyo kwa majirani kwa sababu waswahili walishasema USILOLIJUA NI SAWA NA USIKU WA KIZA..
Maisha ya chuo kwa lucky yalisonga mbele, maryam, Tunu na amina waliamua kumuacha kama alivyo wao wakaendelea na ya kwao, walimtoa thamani na kumuona mjinga asiejua kitu na uenda ametoka shamba ( kijijini) ndo maana anakuwa hachangamuki, ila lililokuwa moyoni mwake hakuna alieweza kulifahamu, na alikubali kuonekana mjinga mbele ya wanaojiona wajanja ili maisha yake yaweze kusonga mbele..

" Rafiki yangu namuonea huruma sana huyu mwenzetu, yani anaishi kama mtu wa kijijini kimandazi mandazi tu sijui yukojee,, msiiiiu. Asubuhi ya jumaa tatu lucky akiwa bafuni anakoga kujiandaa kuingia kwenye kipindi ambapo wao walishajiandaa, Tunu alisema na wenzake namna anavyomchukulia lucky kwa kipindi hicho mbali na nyuma alivyokuwa akimueshimu.

" Si bora mandazi hayachachi, ila Achana nae mshamba huyo, ukimuita haitiki, ukimsemesha anajibu shot, ukimuomba hiki mpaka atake, ana nini kwani hadi tumbembeleze bhana, uzuri wa kutuzidi hana, akituzidi sehemu nyingine tu lakini si face, tufanye yetu tumpoezee aishi kivyake. Alidakia amina.
" mi nlizani mnankalisha chini kusema vitu vya maana kumbe ni huyu chapati, achaneni nae bhana. Kila mmoja mzuri humu ndani na kila mtu nyodo anaziweza, ametunyodoa tumnyodoe, tena sasa hivi niwakupewa visa mpaka chumba akihame hiki. Twendeni class. Alidakia maryam. 

" hhhhhmmmmm. Aliguna tunu, kumbe na wewe umo?. Walinyanyuka na kicheko kila mmoja akabeba mkoba wake na kwenda darasani. lacky alitoka bafuni akiwa na khanga moja mwilini akakaa kitandani na kujifuta futa maji, hakukaa dakika akanyanyuka na kusogea kwenye kioo kujiangalia mwili wake wote ulivyo. Alivuta mafuta aina ya lotion akajipaka baadhi ya sehemu za mwili wake, alipomaliza aliitoa khanga mwili ukabaki utupu kisha akavaa nguo za ndani zilizokuwa kwenye henga.. 

Alimaliza kwa nguo za chuo akabeba mkoba na kutoka ndani, hadi anafika darasan hakuna alieweza kumpa hi kwa sababu ya kusikojulikana sana na watu, kwa alivyokuwa anajiweka hakuna aliweza kumzoea kwani hata mbinu ya kumuingia haikuwepo, wapo wanaume waliojifanya midomo mirefu kutaka kuingiza mistari ya kumtongoza kutokana na uzuri wa mvuto aliokuwa nao kuanzia sura hadi maumbile, lakini walijikuta wanashindwa na kujionea aibu namna ambavyo lucky hakutaka upumbavu..

NINI KITAENDELEA KATIKA EPSODE YA PILI ? Kesho saa tano kamili pita katika yetu hii ya Bongo Swaggz itakuwa tayari imepostiwa. Tafadhali Share na Marafiki Wapenda Stori Ili Wasome Hii Pia.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.