Siku 30 Zimebaki Diamond Platinumz na Zari Kulitikisa Jiji la Dar es Salaam na Nchi Nzima - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Siku 30 Zimebaki Diamond Platinumz na Zari Kulitikisa Jiji la Dar es Salaam na Nchi Nzima

Wachumba wa Zamani Diamond Platinumz na Zari wanatarajia kuandika historia nyingine kama ilivyo kawaida yao pale uwanja wa uhuru ambapo kutakuwa na matukio mengi sana ikiwemo album ya mwanamuzi Diamond Platinumz "A boy from Tandale" ambayo kwa tukio la kuzindua inataraji kuuza nakala 30,000 za mwanzo huku kukiwa na kiingilio kuwaona wasafi wote wakiongozwa na Diamond Platinumz.

Hata hivyo waandaaji wa tukio hili walishaomba uwanja wa taifa lakini wameambiwa utakuwa na matumizi hivyo wamepewa uwanja wa uhuru kwani kwa makisio yao waliona uwanja wa uhuru hautotosha kabisa lakini Plan imekuwa ni kufanya tukio hilo kila mkoa kwa kiingilio ambacho hakitasababisha watu kushindwa kupumua uwanjani.

Katika siku hiyo kutakuwa na tukio lingine kubwa zaidi ambalo sitaliweka hapa kwa sababu za kibiashara lakini joto la tukio hilo litapanda zaidi ikifika march kwani kuna mengi zaidi yatatangazwa kuhusu Diamond na kuwaacha wengi midomo wazi.

Kikubwa zaidi ni kuwa tamasha hili hadi sasa linagombewa na kampuni kubwa mbili ambazo zinataka kuweka matangazo mule ndani ya uwanja siku ya tamasha ambalo bila shaka litaweka historia.


Wana jamvi kwa leo nawajuza haya tuu lakini mkumbuke kuwaona Diamond na Zari safari hii ni kwa pesa si bure tena.

Hakikisha Unapakua App yetu maana Tutakuwa Tunatoa Habari Za Diamond na Zari Live Kila Zinapotokea >>Bofya Hapa<<  KuDownload App Yetu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.