Sababu ya Kupotea kwa Nicki Minaj Mitandaoni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sababu ya Kupotea kwa Nicki Minaj Mitandaoni

Nicki Minaj amekuwa kimya kwenye mitandao ya kijamii kwasababu anataka kuifanyia kazi albamu yake ya nne bila usumbufu wowote wa mitandaoni.

Vyanzo Vilivyopo karibu na Minaj vinasema kuwa Minaj “ana furaha, ana afya nzuri na si mjamzito,” kulingana na TMZ. Rapa huyo haja posti chochote kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram na Twitter tangu Desemba 30 na watu wake wa karibu wanasema kuwa yote hayo anayafanya ile aweze kutoa albamu nzuri kama ile ya mwaka 2014 Pinkprint.

Wendy Williams alizindua kampeni ya kumtafuta kwa msanii huyo katika programu yake.

Kwa sasa, Minaj amekuwa akienda sana studio na wasanii pamoja na maproducer mbalimbali kama Lil Wayne, Mack Maine, na wengine wengi wa kikundi cha Young Money. Minaj ameahidi kuwa hatajihusisha na mtandao wowote wa kijamii mpaka albamu yake ikamilike.

Video ya mwisho Nicki kuonekana ni ya msanii Quavo ‘She For Keeps’

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.