RC Gambo Awapa Wanaume Somo, Ataka Waache Kuwa na Wanawake wa Aina Hii - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

RC Gambo Awapa Wanaume Somo, Ataka Waache Kuwa na Wanawake wa Aina Hii

RC Gambo na Mkewe.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewashauri wanaume nchini waliyo kwenye mahusiano na wanawake ambao hawana mawazo ya kupambana na hali ya uchumi kwa sasa, kujiondoa mara moja kwenye mahusiano hayo kwani ni hatari kwao kwa maisha ya baadae.

Gambo amesema kama mwanaume unataka uwe na uchumi mzuri kwa kipindi hiki ni bora ukaachana na wanawake wanaopenda starehe na kuwa na mwanamke mwenye kutoa ushauri namna gani ya kujikwamua katika maisha haya ya sasa ambayo watu wengi wanalalamika kuwa ni magumu.

“Mwanaume Kama unania ya dhati kuwa na economic freedom in this tough economy basi inatakiwa uepukane na wale wanawake aina ya “Babe nina njaa, nibebee Pizza au Chips kuku asisahau kuweka mayonaise” au “Babe simu Iphone X imetoka naomba ninunulie”. Achana na huo ujuha…Badala yake pata mwanamke aina ya “Babe umekula au unataka nikupikie chakula gani leo” au “Babe ni nini future yako naona hujaweka vizuri vipaumbele vyako”. Spidi ya mwanaume kuwa na maendeleo na hatimae kushinda uhuru wa kiuchumi inategemeana sana na aina ya mwanamke uliyenae,“ ameeleza Mhe. Gambo kwenye ukurasa wake wa Twitter na kumuelezea mwanamke bora wa kuoa.

“Mwanamke bora ni Uwekezaji wenye faida kubwa na mwanamke asiejua nafasi yake ni Mzigo na Liability kubwa sana. Na pale upatapo maendeleo usiwe mbahili… usisahau ku-enjoy na mwanamke aliyekua nyuma ya mafanikio yako..” that’s smart dating and how we smart people do.“
ameeleza Gambo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.