Rais Magufuli Aagiza Hatua Dhidi ya Waliosababisha Kifo cha Mwanafunzi Akwilina Akwiline - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rais Magufuli Aagiza Hatua Dhidi ya Waliosababisha Kifo cha Mwanafunzi Akwilina Akwiline

Marehemu Mwanafunzi Akwilina Akwiline

Rais wa Tanzania John Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuchunguza na kuwachukulia hatua waliosababisha kifo cha mwanafunzi wa chuo cha usafirishaji Tanzania, NIT, Akwilina Akwiline.

"Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT). Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu. Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili," Rais Magufuli aliandika kwenye mtandao wa Twitter.

Mwanafunzi huyo ambaye jina lake na picha vilisambazwa katika mitando ya kijamii alipigwa risasi akiwa ndani ya basi dogo maarufu kama daladala jijini Dar es salaam, siku ya Ijumaa majira ya jioni, ikiwa siku moja kabla ya uchaguzi mdogo wa eneo bunge la kinondoni kufanyika.

Walioshuhudia wanasema kuwa maafisa wa polisi walitumia vitoa machozi na risasi katika harakati za kuwatawanya mamia ya wafuasi wa chama cha Chadema waliokuwa wakiandamana hadi afisi za tume ya uchaguzi.

Wakati huo huo mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP), wamemtaka waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba kujiuzulu kutokana na tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Akwilina Akwiline.

Taarifa zaidi pia zinasema kuwa polisi 6 wamekamatwa kwa tuhuma za kutumia risasi za moto wakati wa uchaguzi mdogo mjini Dar es Salaam.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.