Queen Darleen: Mimi ni Bikra, Natongoza Mume wa Mtu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Queen Darleen: Mimi ni Bikra, Natongoza Mume wa Mtu

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB, Queen Darleen ameshangaza watu wengi baada ya kusema kuwa yeye ni mwanamke bikra kitu ambacho hakiwezekani kwani tayari ana mtoto.

Queen Darleen alifunguka hayo alipokuwa anafanya Interview na LilOmmy kwenye kipindi cha The playlist ambapo aliulizwa status ya Mahusiano yake ya kimapenzi maana haijulikani kwani Kumekuwa na tetesi anatoka na msanii Mbosso wa WCB.

Queen Darleen amefunguka kuwa yeye sio mtu wa kuona aibu yaani akikolea kwa mwanaume akiona hatongozwi basi mwenyewe hujiongeza na kutongoza huyo mwanaume bila uoga wowote na ameshatongoza wanaume wengi huku asilimia kubwa ni waume za watu.

"Mimi bikra kwanza na kuhusu kumzaa mtoto wangu Rooney Mungu kanibariki tu”.

Lakini pia Queen Darleen aliwekwa kitimoto kuhusu tukio lililotokea ambapo Baba mtoto wake alizaa na rafiki yake watoto wawili lakini bado ameendelea kuwa na urafiki na huyo mke mwenzake ambapo alifunguka haya:

"Unajua mimi ni mtu wa dini sana na ninaheshimu dini yangu na dini inaruhusu mwanaume kuoa hata wanawake wanne lakini sikubahatika kuolewa kwanini nimnunie yeye na kama nina uwezo wa kutembea na mwanaume wa mtu kwanini nishindwe kumruhusu mwanaume wangu awe na mtu mwingine”.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.