Nay wa Mitego ni Bingwa wa Kukata Maun, Afunguka Haya - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego ni Bingwa wa Kukata Maun, Afunguka Haya

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Nay wa Mitego amedaiwa mbali ya kuwa na kipaji cha kuimba na kuchana lakini pia ni fundi mkubwa sana wa kukata mauno.

Ney wa Mitego aliyetoa ngoma yake mpya siku ya jumatatu inayoenda kwa jina la ‘Mikono juu’ ameonekana kwenye video ya nyimbo hiyo akikata mauno balaa ambayo yamezoeleka kuonekana kwa msanii kama Bob Junior lakini sio msanii mgumu wa hip hop kama Nay wa Mitego.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Nay amesema yeye ndio aliyemwambia director ashoot hiyo sehemu anayokata mauno maana ni lazima ufanye kitu tofauti kila siku:

"Mimi ndio nilimwambia Nicholaus achukue kile kipande nikiwa napiga uno kidogo lazima ufanye kitu ambacho mtu hatarajii kama utafanya ili mradi kilete utofauti na ndio maana leo hii tupo hapa tunazungumzia vile viuno vyangu kwenye video unajua siku nyingine huwa tunafanya chumbani lakini sahivi tumeamua kuvileta huku ili angalau watu nao wajue sio kwamba hatuwezi hapana tunaweza kujaribu na kufanya utofauti kidogo inaruhusiwa ili kusaidia katika kuleta chachu na kachumbari kwenye kazi na ndio maana sahivi tunazungumzia kile kitu ambacho kipo kwenye ile kazi ni cha tofauti na hakuna mtu aliyekuwa ametarajia kuona mauno yangu"

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.