Nay wa Mitego Afunguka ''Sina Tatizo na Alikiba, Mwenyewe Nina Timu True Boy'' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego Afunguka ''Sina Tatizo na Alikiba, Mwenyewe Nina Timu True Boy''

Msanii wa muziki Bongo, Nay wa Mitego amesema hana beef na Alikiba na wala hana timu yoyote katika muziki.

Nay ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Mikono Juu’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa yeye na Alikiba hawana tatizo lolote na walishafanya hadi wimbo ila haukutoka

“Sina tatizo na Alikiba utimu wao haunihusu, mimi mwenye nina timu True Boy,” amesema Nay wa Mitego.

“Watu hawajui tu, nilishawahi kufanya ngoma na Alikiba, kitambo sana kabla sijawa mkubwa kiasi hiki, haikutoka kabisa, nakumbuka kipindi hicho hata Alikiba hakuwa Alikiba huyu alikuwa Alikiba wa Cinderela mimi nilikuwa nimetoa wimbo unaitwa Itafahamika,” amesisitiza.

Sababu ya wengi kuamini kuwa Nay wa Mitego hana maeleweno mazuri na Alikiba ni kutokana kipindi cha nyuma alikuwa karibu sana Diamond hadi kupelekea kufanya kolabo mbili ‘Muziki Gani, Mapenzi Pesa’, hivyo wengi kuamini yeye ni timu Diamond.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.