Mwasiti Amejifunza Kuwa na Mahusiano ya Siri Kutoka kwa AY - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mwasiti Amejifunza Kuwa na Mahusiano ya Siri Kutoka kwa AY

Mwanamuziki Mwasiti amefunguka sababu ya kufanya siri mahusiano yake ya kimapenzi.

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Kaa Nao’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa hapendi kumuweka wazi mpenzi wake ila pindi atakapoolewa ndipo watu wataweza kumuoana.

Mwasiti ameendelea kwa kusema kuwa amevutiwa na AY kwa namna alivyofanya mahusiano yake siri hadi alipofikikia kipindi cha kukaribia kufunga ndoa ndipo akayaweka wazi.

“Watu mmeanza kumjua girl friend wa Ambwene mwishoni mwishoni huku ambapo sasa nipo tayari kuoa halafu ndoa pap!, kwa hiyo yaani ndio nayataka hayo maisha,” amesema Mwasiti.

Katika hatua nyingine amezungumzia mipango ya kuolewa mwaka huu kwa kusema ni kitu ambacho kinaweza kutokea.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.