Mtoto Aliyezuiwa Hospitalini kwa Miezi 5 Ameachiliwa Baada ya Bili Kulipwa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mtoto Aliyezuiwa Hospitalini kwa Miezi 5 Ameachiliwa Baada ya Bili Kulipwa

Mama yake mtoto Angel aliambia BBC kuwa maziwa yake yamekauka baada ya kutenganishwa na mtoto wake kwa muda wa miezi mitano.

Mama ameelezea furaha yake baada ya zahanati moja ya binfasi nchini Gabon kumuachilia mtoto wake mchanga baada ya kuzuiliwa kwa miezi kadhaa kutokana na kakosa kulipwa bili ya hospitali

Mama yake mtoto Angel aliambia BBC kuwa maziwa yake yamekauka baada ya kutenganishwa na mtoto wake kwa muda wa miezi mitano.

Kisa hicho kiliishangaza nchi na baadaye akapata msaada kutoka kwa umma.

Bili ya dola 3,630 ililipwa baada ya kampeni kuanzishwa kwa niaba ya familia.

Rais Ali Bongo alikuwa miongoni mwa wale waliotoa mchango wao.

Mkurugenzi wa kliniki hiyo alikamatwa Jumatatu kwa mashtaka ya kumteka nyara mtoto, lakini mashtaka hayo yakaondolewa baadaye.

Angel baadaye aliachiliwa na kuondoka zahanati hiyo iliyo kaskazini mwa mji muu wiki hii.

Mama yake mtoto huyo Sonia Okome aliiambia BBC kuwa alifurahi lakini pia amehusunika kwa kuwa hawezi kumyonyesha mtoto wake kwa sababu maziwa yalikauka.

Pia alilalamika kuwa mtoto huyo hajapewa chanjo yoyote.

-BBC

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.