Man United Yakubali Kichapo Kutoka kwa Newcastle - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Man United Yakubali Kichapo Kutoka kwa Newcastle


Klabu ya soka ya Manchester United leo imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa klabu ya Newcastle United.

Bao pekee katika mchezo huo wa ligi kuu ya soka nchini England uliomalizika jana jioni kwenye uwanja wa Saint James Park limefungwa na Matt Ritchie dakika ya 65.

Kwa upande wa kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameendelea kuwa na rekodi mbaya kwenye uwanja huo akiwa hajawahi kushinda mchezo wowote wa ligi.

Mourinho akiwa na Chelsea na Manchester United kwa sasa amefanikiwa kushinda mechi mbili tu kati ya tisa kwenye uwanja wa St. James Park huku mechi hizo mbili zikiwa ni za kombe la ligi (EFL CUP).

Matokeo ya yanaiacha Manchester United katika nafasi ya pili ikiwa na alama 56 ikiwaacha vinara manchester City wakiwa kileleni kwa alama 72.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.